Na Daniel Sichula – Mahakama, Mbeya
Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Dyness Lyimo ametoa taarifa ya mashauri yaliyosikilizwa, kutolewa maamuzi na ambayo yamehairishwa na Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani kwenye kikao maalum cha kutoa tathmini kwa wadau wa Mahakama walioshiriki vikao hivyo vilivyokua vikisikiliza mashauri ya rufani Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya kwa muda wa siku 12 kuanzia tarehe 25 Novemba 2024.
Aidha, Mhe. Lyimo alisema katika taarifa hiyo kuwa, mashauri 23 yaliyopangwa kusikilizwa awali umefanikiwa kwa asilimia 96 kwa mashauri yote yaliyosikilizwa, mashauri 19 yametolewa maamuzi yakiwemo mashauri ya jinai 12, mashauri ya madai saba (7) na mashauri matatu (3) yanatajiwa kutolewa uamuzi tarehe 13 Disemba, 2024 huku shauri moja (1) limehairishwa baada ya kusikilizwa na kubainika baadhi ya nyaraka kukosekana katika shauri hilo.
Mhe. Lyimo amebainisha kuwa sababu ya kuhairisha shauri hilo ni kutokana na changamoto mbalimbali zilizobainishwa na Jopo katika usikilizwaji wa mashauri, mfano; baadhi ya wadaawa kutokuleta taarifa za nyongeza mapema na kukosekana kwa nyaraka muhimu katika kumbukumbu zao za rufaa na kupelekea kutokamilika kwa shauri hilo.
Naye,
Mwenyekiti wa kikao hicho Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Lugano
Mwandambo akiongoza jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani walioshirikiana
katika usikilizaji na utoaji wa maamuzi wa mashauri hayo aliwashukuru washiriki
wote, Mawakili wa Serikali, Mawakili wa Kujitegemea, Ofisi ya waendesha
mashtaka, Jeshi la Magereza kwa ushirikiano waliutoa katika kipindi chote cha
usikilizaji wa mashauri.
“Nichuke nafasi hii kuwahasa mawakili kwamba, mnapokuja mahakamani muwe mnajiandaa na mnawaanda wateja vyema kwani lolote linaweza kutokea wakati wa usikilizwaji wa mashauri na mjenge tabia ya kufuatulia mashauri yenu kwa Naibu Wasajili wa Mahakama ili kujua nini kinaendelea na kuweza kusaidia kama shauri halijakamilika na lishawekwa kwenye mpango wa usikilizaji liweze kutolewa na kuwekwa lingine hii itasaidia kupunguza mlundikano wa mashauri na kuwapatia haki watu wengine hasa wafungwa walioko magerezani,” alisema Mhe. Mwandambo.
Nao, Majaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Kairo na Mhe. Issa kwa pamoja waliwashukuru wadau wote kwa kutoa ushirikiano na kurahisisha kazi ya usikilizaji wa mashauri na kuupongeza Uongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa mapokezi mazuri, “Mafanikio tuliyopata ni yetu sote bila ushirikiano wenu tusingeweza kufanikisha hili,” alisema Mhe. Kairo.
Wakati
huo huo, Uongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kupitia kwa Jaji Mfawidhi Mhe.
Joachim Tiganga awashukuru na kulipongeza Jopo la Majaji hao wa Mahakama ya Rufani
kwa uchapakazi wao katika kipindi chote cha usikilizaji wa mashauri ya rufani
na kuahidi kufanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika uandaaji na usajili
wa mashauri ya rufani.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Lugano Mwandambo aliyeongoza jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani akifafanua jambo wakati wa kikao hichov na wadau wa Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni