Jumatatu, 30 Desemba 2024

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI SAFARI YA MWISHO YA JAJI KWARIKO

 ·       Jaji Mkuu asema  Jaji Kwariko ameisaidia  Mahakama  kutenda haki bila upendeleo

Na INNOCENT KANSHA, SALUM TAWANI-Mahakama, Kondoa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa Majaliwa amewaongoza watumishi wa Mahakama na Wananchi mjini Kondoa katika safari ya mwisho ya Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko ambaye amezikwa kwenye makaburi ya familia Bicha Wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma leo tarehe 30 Desemba 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa, amesema kuwa Jaji Kwariko alikuwa mtendaji mzuri na ni miongoni mwa majaji wanawake wachache wa Mahakama ya Rufani ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kiutendaji kazi akiwa katika nafasi hiyo, hivyo kutangulia kwake mbele za haki Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehuzunika sana kupata taarifa za msiba huo pia Taifa limepata pengo katika nafasi yake ya ujaji wa Mahakama ya Rufani.

“Marehemu Kwariko alikuwa Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania aliteuliwa na Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwaka 2021, Tume hiyo inafanya kazi kwa karibu zaidi na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa upande wa Serikali. Utendaji wa kazi wa Mhe. Kwariko kama Kamishna wa Tume hiyo kulingana na kama Mwenyekiti wa Tume hiyo  alivyoelezea, sisi kama Ofisi tumeguswa na msiba huu mzito  na kwa hiyo tunaungana na Mhe. Rais kutoa pole kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania, kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na familia kwa ujumla,’’ amesema Waziri Mkuu. 

Naye, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa salamu za pole kufuatia kifo hicho, alimuelezea Marehemu Kwariko kama mtumishi wa Umma aliyetekeleza majukumu yake kwa kuwajali wengine, kwa uaminifu na kwa bidii ya hali ya juu na kwamba, mchango wake kwa Taifa hautasahaulika kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya.

“Kuna wakati Rais wa Marekani Abraham Lincoln aliwahi kusema, ubora wa maisha siyo miaka ambayo unaishi duniani ubora wa maisha ni yale unayowafanyia binadamu wenzako ndiyo watu  wanakukumbuka zaidi unaweza kukaa miaka kumi au  ishirini lakini  unaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya wale waliojaaliwa uhai mrefu kwa hiyo sisi tunamshukuru Mungu kwa uhai wa Mhe. Kwariko umetusaidia sana katika shughuli mbalimbali za kuhudumia wananchi hasa katika kutoa haki bila ya upendeleo,’’ amesema Mhe. Prof. Juma.

Vilevile, Jaji kwariko alikuwa Kiongozi katika ngazi ya Familia, Muhimili wa Mahakama na pia  kwenye Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania, hivyo basi  maeneo yote aliyofanya kazi  yanagusa maisha ya mtanzania  na ndiyo maana huu ni wakati wa kumshukuru Mwenyezi Mungu akumbuke yote mema ambayo Mhe. Kwariko aliyafanya kwasababu daftari la Mwenyezi Mungu halisahu kitu.

“Binadamu kiuhalisia anaweza kusahau mema lakini daftari la Mwenyezi Mungu halisahau na tunamuombea mema mengine ambayo tumeyasahau aweze kuyajumuisha kwenye daftari lake. Unaweza ukawa binadamu na usiwe na utu, lakini Mhe. Kwariko alikuwa na ubidamu na hii inatokana na salaam mbalimbali ambazo nimekuwa nikizipokea zinazoonyesha kwamba alikuwa na ubinadamu na utu,’’ amesema Jaji Mkuu.

Aidha, Mwenyekeiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Jacobs Mwambegele, amesema kuwa, walikuwa wanamuhitaji sana Jaji Kwariko katika kipindi hiki cha uboreshwaji  wa daftari la Kudumu la wapiga Kura  kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania.

“Tume Huru ya Uchaguzi  tumempoteza Marehemu Kamishna Kwariko wakati tukiwa katika mzunguko wa nane wa  zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  na tukisubiri kuingia katika mzunguko wa tisa utakaohusisha mikoa minne  ya Rukwa, Songwe, Njombe na Ruvuma, ilichukua muda kutafakari vipi msiba huu kwa mwenzetu ambae alikuwa nasi bega kwa bega wakati wa Majukumu tunayotekeleza, alitoa ushirikiano mkubwa ambao ndiyo umetufikisha hapa, alihakikisha kuwa, Majukumu ya Tume yanatekelezwa kwa kuzingatia Katiba, Sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa,’’ amesema mwenyekiti Mwambegele.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Barke Mbaraka Sehel, amesema kuwa, Mhe. Kwariko alikuwa mwachama mzuri na  hai hivyo Chama  kinatoa pole kwa ndugu na jamaa wote na ifahamike kuwa mauti kwa binadamu ni fumbo kubwa ila ni jambo la  kumshukuru  Mwenyezi Mungu, kilichobaki ni kumuombea Dua ili kujiandaa na siku ya mwisho kila mmoja wetu  atakapoitwa.

Katika mazishi hayo Viongozi mbalimbali wa Mahakama walihudhuria wakiwemo Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Majaji wa Mahakama Kuu, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Watendaji wa Mahakama, Mahakimu wa ngazi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Kada mbalimbali.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akitoa salaam za pole kwa waombolezaji kwa niaba ya Serikali kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko katika mazishi yaliyofanyika leo tarehe 30 Disemba, 2024 mjini Kondoa mkoani Dodoma.
 
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akitoa salaam za pole kwa waombolezaji kwa niaba ya Serikali kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko katika mazishi yaliyofanyika leo tarehe 30 Disemba, 2024 mjini Kondoa mkoani Dodoma.
 

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisaini Kitabu cha maombolezo alipowasili kushiriki mazishi kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa salamu za pole kufuatia kifo hicho na kutoa nasaha kwa waombolezaji kuwa mfano wa kuigwa na kuacha alama kwenye jamii ili siku moja wakumbukwe kwa mema waliyoyatenda, mazishi hayo yamefanyika mjini Kondoa leo tarehe 30 Disemba, 2024.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyotokana na ratibu ya kuuaga mwili wa marehemu Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa


Watoto wa marehemu wa aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko wakiwa msibani mjini Kondoa. Kushoto ni Abraham na Neema Kwariko.

Mwenyekeiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Jacobs Mwambegele (kulia) akipeana mkono wa pole na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (kushoto) wakati wa msiba huo.

Mtoto Abraham wa marehemu Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko akisoma wasifu.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Barke Mbaraka Sehel akitoa salam za pole kwa waombolezaji kufuatia kifo cha mwanachama wa Chama hicho ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko.

Mwenyekeiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Jacobs Mwambegele akitoa salam za pole kwa waombolezaji kufuatia kifo cha ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) wakiwa wamesimama ikiwa ni ishara ya kutoa heshima wakati wa kuupokea na kuuaga mwili wa marehemu Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga na Katibu wa Chama cha Majaji cha Kuinuana Mhe. Frank Mahimbali akitoa salam za pole kwa waombolezaji kufuatia kifo cha mwanzilishi wa umoja huo wa Majaji ambaye pia alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa huo, Mhe. Rosemary Senyamule (aliyesimama kwenye podium) akitoa salam za pole kwa niaba ya mkoa kwa waombolezaji kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na pia kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko ambaye mazishi yake yamefanyika mjini Kondoa mkoani Dodoma.

Majaji wakiwa wamejipanga mistari miwili wajitayarisha kupokea Sanduku maalum lililobeba mwili wa mpendwa wao ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko ambaye amezikwa kwenye makaburi ya familia Bicha Wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma leo tarehe 30 Desemba 2024.

Majaji wakipokea Sanduku maalum lililobeba mwili wa mpendwa wao ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko ambaye amezikwa kwenye makaburi ya familia Bicha Wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma leo tarehe 30 Desemba 2024.


Sehemu ya waombolezaji walioshiriki mazishi kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa.

Sehemu ya waombolezaji walioshiriki mazishi kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa.

Sehemu ya waombolezaji walioshiriki mazishi kufuatia kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (kushoto) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wakiwa kwenye makaburi ya Bicha alikopumzishwa marehemu Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa. Kushoto anayefuatilia mazungumzo hayo ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma.


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (kushoto) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wakiwa kwenye makaburi ya Bicha alikopumzishwa marehemu Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye pia alikuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania Mhe. Mwanaisha Athuman Kwariko mjini Kondoa. Wa pili kushoto anayefuatilia mazungumzo hayo ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma na Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Augustine Mwarija.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa aliyeshika koleo akiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kwenye makaburi ya Familia Bicha Kondoa Mjini mkoani Dodoma.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma aliyeshika koleo akiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kwenye makaburi ya Familia Bicha Kondoa Mjini mkoani Dodoma.

Mwenyekeiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Jacobs Mwambegele  aliyeshika koleo akiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kwenye makaburi ya Familia Bicha Kondoa Mjini mkoani Dodoma.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani aliyeshika koleo akiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kwenye makaburi ya Familia Bicha Kondoa Mjini mkoani Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel aliyeshika koleo akiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kwenye makaburi ya Familia Bicha Kondoa Mjini mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimpa mkono wa pole mtoto wa Marehemu Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko mara baada ya swala ya mazishi.

(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni