Na FAUSTINE
KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 14 Januari, 2025 amemkabidhi nyenzo za
kufanyika kazi Mhe. Janeth Boaz Kinyage baada ya kuteuliwa kuwa Hakimu
Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Hafla hiyo imefanyika
katika Ofisi ya Jaji Mkuu kwenye jengo la Mahakama ya Rufani Tanzania jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Mahakama, akiwemo Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani.
Viongozi wengine wa
Mahakama waliohudhuria hafla hiyo ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Obadia
Bwegoge, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya, Msajili wa
Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Tiganga Tengwa, Naibu Wasajili pamoja na ndugu wa karibu wa Mhe. Janeth.
Akizungumza katika hafla
hiyo fupi, Jaji Mkuu wa Tanzania amempongeza Hakimu Mfawidhi huyo kwa kupewa
heshima ya kuwa Kiongozi wa Mahakama katika ngazi ya Mkoa wa Morogoro, kati ya
Mikoa mikubwa yenye maeneo makubwa.
“Kwa sababu umepewa nyenzo
pekee yako, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania atatayarisha siku ambayo wewe
na wengine mtapata mafunzo elekezi yatakayokuwezesha kufanya kazi. Nakupongeza
sana, nikutakie kila heri,” Mhe. Prof. Juma amemweleza Mhe. Janeth.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Janeth Boaz Kinyage (juu na chini) kwa unyenyekevu mkubwa akipokea nyenzo za kazi kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto). Anayeshuhudia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini nyaraka mbalimbali kabla ya kuzikabidhi kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogorio, Mhe. Janeth Boazi Kinyage (hayupo kwenye picha).
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya akitoa maelezo mafupi kuhusu hafla hiyo.
Viongozi wa Mahakama waliohudhuria hafla hiyo. Kutoka kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Obadia Bwegoge, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Tiganga Tengwa.
Viongozi wengine wa Mahakama waliohudhuria hafla hiyo (juu na chini) wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanajiri.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Janeth Boaz Kinyage (kulia). Chini akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (kushoto) na Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Obadia Bwegoge (kulia).
Mhe. Janeth Boaz Kinyage (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mahakama waliohudhuria hafla hiyo. Picha chini akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa pili kushoto) pamoja na ndugu zake wa karibu.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Janeth Boaz Kinyage (juu na chini) akipongezwa na ndugu zake baada ya kukabidhiwa nyenzo za kazi.
Mhe. Janeth Boaz Kinyage
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni