Jumanne, 21 Januari 2025

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA AFARIKI DUNIA


TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Bw. Juma Hijja Kabogota aliyekuwa akihudumu kama Afisa Ugavi Mwandamizi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, marehemu Juma alikutwa na umauti mnamo jana tarehe 20 Januari, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kipatiwa matibabu. Marehemu Juma alianza kuugua tangu Aprili mwaka 2021 hadi 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya kuugua kwa vipindi tofauti na kulazwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Manispaa ya Kigamboni (Changanyikeni - Chekechea mtaa wa Mnarani). Aidha, mazishi ya marehemu yatafanyika tarehe 21 Januari, 2025 majira ya Saa Kumi Alasiri huko Kigamboni.

Marehemu Juma Hijja Kabogota aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tarehe Mosi Agosti, mwaka 2009 kama Afisa Ugavi Kituo cha Makao Makuu ya Mahakama jijini Dar es salaam, kuanzia mwaka 2009 hadi 2019. Mnamo mwaka 2019 hadi 2025 hadi umauti unamfika marehemu Juma alikuwa akihudumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi jijini Dar es Salaam akiwa ni Afisa Ugavi Mwandamizi.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.

INALILLAH WAINA ILLLAH RAJIUN.

Marehemu Juma Hijja Kabogota enzi za uhai wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni