TANZIA
Mahakama ya Tanzania
inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Bw. Juma Hijja Kabogota aliyekuwa
akihudumu kama Afisa Ugavi Mwandamizi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni
ya Ardhi jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, marehemu Juma
alikutwa na umauti mnamo jana tarehe 20 Januari, 2024 katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili alipokuwa amelazwa kipatiwa matibabu. Marehemu Juma alianza kuugua
tangu Aprili mwaka 2021 hadi 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya kuugua kwa
vipindi tofauti na kulazwa.
Taarifa hiyo imeeleza
kuwa, msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Manispaa ya Kigamboni (Changanyikeni -
Chekechea mtaa wa Mnarani). Aidha, mazishi ya marehemu yatafanyika tarehe 21
Januari, 2025 majira ya Saa Kumi Alasiri huko Kigamboni.
Marehemu Juma Hijja
Kabogota aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tarehe Mosi Agosti, mwaka 2009 kama
Afisa Ugavi Kituo cha Makao Makuu ya Mahakama jijini Dar es salaam, kuanzia
mwaka 2009 hadi 2019. Mnamo mwaka 2019 hadi 2025 hadi umauti unamfika marehemu
Juma alikuwa akihudumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi
jijini Dar es Salaam akiwa ni Afisa Ugavi Mwandamizi.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.
INALILLAH WAINA ILLLAH RAJIUN.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni