Marehemu Andrea Hamisi Mpochele enzi za uhai wake.
Mahakama
ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bw. Andrea Hamisi Mpochele
aliyekuwa akihudumu kama Afisa Hesabu Msaidizi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Lindi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu MKazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela
amesema marehemu alifikwa na umauti jana tarehe 19 Mei, 2025 katika hospitali
ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict Ndanda iliyopo Mkoa wa Mtwara alipokuwa amelezwa
akipatiwa matibabu.
Taarifa
ya Mtendaji huyo imeeleza kuwa msiba upo nyumbani kwa Marehemu kijiji cha
Lisekese wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara, Aidha mazishi yatafanyika siku ya
tarehe 21 Mei, 2025 muda wa saa 7:00 Mchana.
Marehemu Andrea Hamisi Mpochele aliajiriwa na Mahakama
ya Tanzania tarehe 2 Aprili mwaka 1990 kama Masjala
Msaidizi wa Mahakama III katika
Mahakama ya Wilaya ya Lindi na baada ya hapo alijiendeleza katika fani ya uhasibu na ilipofika tarehe 01 Oktoba 2021 alibadilishwa kada na kuwa Msaidizi wa
Hesabu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi mpaka umauti ulipomfika.
Mahakama
ya Tanzania inaungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuomboleza msiba huo wa kuondokewa
na mpendwa wetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni