Jumatatu, 8 Septemba 2025

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA AFARIKI DUNIA

Marehemu Paskalia Msalila Ndunguru enzi za uhai wake.

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Bi. Paskalia Msalila Ndunguru aliyekuwa akihudumu Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kama Msaidizi wa Ofisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 08 Septemba, 2025 na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga, Bw. Jumanne Muna, marehemu Paskalia alifikwa na umauti ghafla tarehe 06 Septemba, 2025.

Bw. Muna amesema kuwa, Mamlaka za uchunguzi bado zinaendelea na uchunguzi kujua nini chanzo cha kifo cha mtumishi huyo.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu Paskalia Msalila Ndunguru.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni