Jumatano, 4 Februari 2026

JAJI KIONGOZI AKUTANA NA VIONGOZI WA TMJA TAWI LA MASJALA KUU

Na. Mwandishi Wetu-Mahakama.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Mahakama Kuu Tawi la Masjala Kuu, amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Tawi hilo leo tarehe 4 Februari, 2026 Ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma na kuweka mikakati mbalimbali itakayokiwezesha Chama kuweka misingi imara itakayoacha alama chanya isiyosahaulika kwa ajili ya wanachama wa sasa na wajao.

Kufuatia misingi hiyo iliyowekwa, Mhe. Dkt. Siyani kama mlezi ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa uongozi huo ili kuwezesha utekelezaji wa mikakati hiyo itakayowezesha usimamizi bora wa Chama na msaada kwa wanachama na jamii kwa ujumla.


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA)Mahakama Kuu Tawi la Masjala Kuu, akizungumza wakati alipotembelewa ofisini kwake na viongozi wa TAMJA Tawi la Mahakama Kuu Masjala Kuu, leo tarehe 4 Februari, 2026 Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodooma 

Viongozi wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA)Mahakama Kuu Tawi la Masjala Kuu, wakiwasilisha mikakati ya Chama hicho kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani ambaye pia ni Mlezi wa Chama hicho. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA)Mahakama Kuu Tawi la Masjala Kuu, Mhe. Desidery Kamugisha ambaye pia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, akiwasilisha mikakati ya Chama hicho kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (hayupo pichani) ambaye pia ni Mlezi wa Chama hicho. 

Sehemu ya viongozi wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Mahakama Kuu Tawi la Masjala Kuu.

Katibu wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Mahakama Kuu Tawi la Masjala Kuu, Mhe. Kifungu Mrisho Kariho ambaye pia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, akichangia mada wakati wa kikao hicho  mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (hayupo pichani) ambaye pia ni Mlezi wa Chama hicho. 
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (aliyesimama katikati) ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Mahakama Kuu Tawi la Masjala Kuu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama hicho.

PICHA NA INNOCENT KANSHA - MAHAKAMA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni