Na. Christopher Msagati-Mahakama, Manyara
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara Mhe. Ilvin C. Mugeta
ameahidi kutoa ushirikiano katika ufanikishaji wa shughuli za maendeleo nchini
ambazo zinafanyika kwa ajili ya mustakabali wa ustawi na maendeleo ya Taifa.
Mhe.
Mugeta ameyasema hayo jana tarehe 02 Februari, 2026 katika maadhimisho ya Siku
ya Sheria Nchini kwa Mwaka 2026 ambayo Kikanda yameadhimishwa katika viwanja vya
Mahakama Kuu Manyara wilayani Babati mkoani Manyara.
“Mazingira
mazuri ya upatikanaji wa haki yanasaidia katika ustawi wa Taifa na maendeleo
yake kwa ujumla, tumebaini kuwa mashauri yakikaa mahakamani kwa muda mrefu,
wananchi hukosa muda wa kushiriki katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii,
hivyo maendeleo huzorota…
…Mahakama
Kuu Kanda ya Manyara, itaendelea kuboresha zaidi huduma hii ya msingi kwa
kuendelea kutoa hukumu zenye weledi lakini pia kwa kufupisha muda wa kusikiliza
mashauri na hivyo kuwawezesha wananchi kupata muda wa kufanya shughuli zao za
kiuchumi kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu,” alisema Mhe. Mugeta.
Akiongea
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela
Kaganda alisema Serikali itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na Mhimili wa
Mahakama kwa kuwezesha upatikanaji wa mazingira rafiki ya utendaji kazi ikiwemo
kuipatia Mahakama mahitaji ya muhimu ambayo yataiwezesha Mahakama kufanya kazi
zake pasipo matatizo yoyote.
“Kaulimbiu
ya maadhimisho ya Siku ya Sheria Mwaka huu, inaonesha jinsi ambavyo maendeleo
ya taifa lolote yanavyostawi kwa kutegemea upatikanaji wa Haki na Amani. Aidha,
Mkoa wetu wa Manyara umegubikwa na wimbi kubwa la makosa ya ukatili wa kijinsia
na mengineyo mengi ambayo yanakwamisha maendeleo ya taifa letu kwa namna moja
ama nyingine. Ninaviasa vyombo vya Haki Jinai kuendelea kushirikiana kwa pamoja
ili tuweze kuwa na Taifa lenye nidhamu na maendeleo,” alisema Mhe Kaganda.
Kwa
upande wake, Bw. Lameck Butuntu ambaye ni mwakilishi wa Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali alisema, Mahakama ina mchango mkubwa katika kuwezesha uwekezaji
kutoka kwa watu mbalimnbali wa ndani na hata nje ya nchi.
“Wawekezaji
katika miradi mbalimbali ya kiuchumi hupenda kuwekeza katika maeneo ambayo kuna
mazingira salama yasiyokuwa na migogoro lakini pia ambayo yana tija katika upatikanaji
bora wa Haki, hivyo ni rai yetu kuwa Mahakama iendelee kufanya kazi kwa bidii
na kwa kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma hususani kwa kujenga miundombinu
wezeshi ya kuwavutia wawekezaji,” alisema Bw. Butuntu.
Mahakama
Kuu Kanda ya Manyara imeungana na Mahakama za Kanda na Mikoa mingine nchini
kuadhimisha Siku ya Sheria kwa Mwaka 2026, yenye Kaulimbiu isemayo “Mchango wa Mahakama katika Ustawi na
Maendeleo ya Taifa” kaulimbiu ambayo imesisitiza umuhimu wa Mhimili wa
Mahakama katika ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na Kijamii kwa kuzingatia Dira
ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. Ilvin Mugeta akitoa hotuba ya
Siku ya Sheria Nchini kwa Wananchi na wadau waliohudhuria katika viwanja vya
Mahakama Kuu Manyara.
Mwakilishi
wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Manyara Bw. Lameck Butuntu
akitoa hotuba yake ya Siku ya Sheria Nchini kwa Mwaka 2026 mbele ya Wananchi na
wadau waliohudhuria katika viwanja vya Mahakama Kuu Manyara.
Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini kwa Mwaka 2026 katika viwanja vya Mahakama Kuu Manyara.
Mkuu
wa Wilaya ya Babati Mhe Emmanuela Kaganda akitoa hotuba yake kwenye Maadhimisho
ya Siku ya Sheria Nchini kwa Mwaka 2026 katika viwanja vya Mahakama Kuu
Manyara.
1. Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. Ilvin Mugeta akiwa na Meza Kuu
katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kwa Mwaka 2026, (wa pili kulia) ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. Devotha Kamuzora, kulia ni Mwakilishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Mkoa wa Manyara Bw. Lameck Butuntu, (wa tatu kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Kaganda, wa pili kushoto ni Jaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. Nenelwa Mwihambi na . wa kwanza kushoto ni Bw. Tadei Lister
ambaye ni Mwenyekiti wa Mawakili wa Kujitegemea Mkoa wa Manyara.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara Mhe. Ilvin C. Mugeta
akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa katika maadhimisho ya Siku ya Sheria
Nchini mwaka 2026.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni