Alhamisi, 2 Februari 2017

KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA AFUNGA RASMI MAONYESHO YA WIKI YA ELIMU YA SHERIA



Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.  Prof. Ibrahim Juma, akihutubia baadhi ya watumishi na wananchi waliofika katika sherehe za kufunga rasmi Maonyesho ya Wiki ya Sheria yalioanza kufanyika kuanzia Januari, 28, 2017 hadi Februari 1, 2017.


Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiendelea kuhutubia, amewaasa Watumishi wote wa Mahakama pamoja na Wadau wa Mahakama kuwatumikia wananchi kwa moyo wa dhati na kwa kujituma.

Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiendelea kuhutubia, amewaasa Watumishi wote wa Mahakama pamoja na Wadau wa Mahakama kuwatumikia wananchi kwa moyo wa dhati na kwa kujituma.
 Baadhi ya watumishi na wananchi wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu mapema leo Februari 01, 2017 alipokuwa akifunga rasmi Maonyesho ya Wiki ya Elimu ya Sheria.
Watumishi wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu.
Mbali na kufunga Maonyesho , Mhe. Kaimu Jaji Mkuu aliwapatia Kompyuta Mpakato 'laptop' baadhi ya Mahakimu 7 kati ya 58, kwa ajili ya utendaji kazi wa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwasaidia Wahe. Mahakimu kutoa nakala za hukumu kwa wakati.
Haimu Mkazi Mfawidhi- Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akifurahia kompyuta yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mhe. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni