Ijumaa, 24 Februari 2017

WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA MAHAKAMA WASAINI MIKATABA YA KAZI


Na Mary Gwera
Wakuu Wa Idara na Vitengo wa Mahakama ya Tanzania leo  wamesaini Mikataba ya Kazi kwa ajili utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama.

Zoezi hilo fupi la utiaji sahihi limefanyika mapema leo Februari 24, katika Ukumbi wa Maktaba wa Mahakama ya Rufani (T) ikishuhudiwa na Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti ya Mahakama.

Katika muendelezo wa utekelezaji wa Mpango Mkakati huo, jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kufikia malengo yaliyowekwa katika mpango huo wenye lengo kuu la kuboresha huduma ya upatikanaji haki nchini.

Zoezi hilo maalum la utiaji sahihi Mikataba ya kazi limefanyika kati ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga, Msajili Mkuu, Mhe. Katarina Revokati pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wanaosimamia utekelezaji wa malengo ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania 2015-2020.

Akizungumzia zoezi hili muhimu, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Utekelezaji wa Shughuli za Mpango Mkakati wa Mahakama pamoja na Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama, Mhe. Zahra Maruma alisema kuwa Mahakama imejiwekea mfumo wa utekelezaji wa Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho kwa Mfumo wa Matokeo Makubwa sasa, (BRN).

“Zoezi lililofanyika leo linalenga katika upimaji wa Viashiria muhimu tulivyokubaliana katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama,” alieleza Mhe. Maruma. 

Wakuu wa Idara na Vitengo waliokabidhiwa Mikataba hiyo ni Msajili-Mahakama ya Rufani (T), Msajili-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mkurugenzi wa Utawala, Menejimenti ya Rasilimali Watu, Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri, Mkurugenzi Msaidizi- Ukaguzi, Maadili na Malalamiko na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.

Wengine ni Kitengo cha Usimamizi wa Majengo na Idara ya TEHAMA.
Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama vilizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Septemba 21, 2016. 
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (katikati) akimuonesha kitu Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati (kulia) walipokuwa wakisaini Mikataba ya kazi ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taasisi, kushoto ni Msajili-Mahakama ya Rfani (T), Mhe. John Kahyoza.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akisaini Mkataba wa kazi kwa ajili ya kumkabidhi Msajili-Mahakama ya Rufani (T).
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (katikati) akimkabidhi Mkataba wa kazi Msajili-Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza (kushoto), anayeshuhudia ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati.
Msajili-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta akikabidhiwa Mkataba wa kazi na Mtendaji Mkuu pamoja na Msajili Mkuu mapema leo Februari 24, 2017.
Viongozi wakiendelea na zoezi la uwekaji sahihi likiendelea, kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu- Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward Nkembo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu akipokea Mkataba wa Kazi kutoka kwa Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu.
Zoezi la uwekaji saini likiendelea, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Bw. Nurdin Ndimbe.
Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wakimkabidhi Mkataba wa Kazi, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama.
Mkurugenzi Msaidizi, Ukaguzi, Maadili na Malalamiko, Mhe. Happiness Ndesamburo akionesha Mkataba wa kazi aliokabidhiwa kwa ajili ya utekelezaji mapema leo. katikati ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, na kulia ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti ya Mahakama wakiwa katika kikao hicho mapema leo, ambapo shughulia ya uwekaji sahihi wa mikataba ilifanyika.
Sehemu ya baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama wakiwa kikaoni.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni