Jumanne, 28 Machi 2017

WAHASIBU NA WATENDAJI WA MAHAKAMA-PWANI WAHIMIZWA KUFUATA TARATIBU ZA FEDHA

Watumishi wa Mahakama hususani Wahasibu na Watendaji wa Mahakama wameaswa kufuata taratibu na sheria za fedha katika kufanya malipo mbalimbali.

Hayo yalisema na Mkaguzi wa Ndani- Mahakama, Bi. Augustina Kimati katika kikao cha pamoja kati yake na Watumishi hao kilichofanyika Machi 24, mwaka huu Kibaha-Pwani.

Mbali na kuwasisitiza juu ufuataji wa taratibu stahiki za malipo, Bi. Kimati aliwapa Watendaji hao mbinu mbalimbali za kufuata ili kuepuka hoja zisizo na msingi hasa pale watakapotembelewa na Wakaguzi wa nje.

Katika kikao hicho, Bi. Kimati aliwafunda Wahasibu na Watendaji kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kufuata taratibu za fedha  na kuwasisitiza juu ya kufuata Sheria ya Manunuzi Serikalini na ‘Public Finance Act.’
Mkaguzi wa Ndani-Mahakama ya Tanzania, Bi. Augustina Kimati (kulia) akiwa na Naibu Mtendaji Mkoa wa Pwani, Bi. Stumai Hozza (kushoto) wakiwa katika kikao cha Ukaguzi, Kibaha-Pwani.
Watendaji na Wahasibu wa Mahakama ya Wilaya na Mkoa wa Pwani wakiwa katika kikao cha Ukaguzi kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni