Alhamisi, 25 Mei 2017

JAJI KIONGOZI AANZA ZIARA YA KIKAZI, MAHAKAMA KUU KANDA YA SONGEA NA MTWARA


Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Songea, Mhe. David Mrango (wa kwanza kushoto) pamoja na watumishi na Viongozi wengine wa Serikali wakisubiri kumlaki Mhe. Jaji Kiongozi kwa ajili ya kuanza ziara katika Kanda hiyo.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akisalimiana na Maafisa wa Mahakama pindi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea kwa lengo la kujionea hali ya utoaji haki katika Kanda hiyo na Kanda ya Mtwara pia, wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Songea, Mhe. David Mrango.
Salaam
 Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Ndunguru (kulia) pindi walipokuwa wakisubiri kumlaki Mhe. Jaji Kiongozi tayari kwa kuanza ziara.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akisaini kitabu cha wageni pindi alipowasili, Mahakama Kuu-Kanda ya Songea.
(Picha na Lydia Churi, Songea)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni