Alhamisi, 29 Juni 2017

KAIMU JAJI MKUU, MHE. PROFESA IBRAHIM JUMA AWAPOKEA NA KUWAKUBALI MAWAKILI 248.

 
Kaimu Jaji Mkuu  wa  Tanzania,  Mhe. Profesa Ibrahim  Juma(katikati)  akiwa katika picha ya pamoja  na Mawakili Wapya mara baada ya  kuwapokea  Mawakili wapya 248 walioapishwa na kukubaliwa katika sherehe  ya 56 (1986-2017).
Pichani ni  baadhi  ya wananchi wakiwa katika hafla hiyo.
  Kaimu Jaji Mkuu  wa  Tanzania,  Mhe. Profesa Ibrahim  Juma(katikati)  akiwa na baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu ya Tanzania wakitoa heshima kama ishara ya kuwapokea Mawakili wapya 248 walioapishwa na kukubaliwa.
 

Baadhi ya waandishi wa habari  wakizungumza  na Kaimu Jaji Mkuu  wa  Tanzania,   Mhe. Profesa Ibrahim  Juma (ambaye  hayupo pichani).


Baadhi ya mawakili hao, wakiwa wamesimama katika hatua ya kuapishwa.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu   wakiwa katika  hafla hiyo .
     Kaimu Jaji Mkuu  wa  Tanzania,  Mhe. Profesa Ibrahim  Juma akizungumza  na  baadhi  ya  waandishi wa habari mara  baada  ya kuwapokea  Mawakili wapya 248 walioapishwa na kukubaliwa leo jijini Dar es salaam.

(Picha   na Magreth Kinabo)

Na Magreth Kinabo

Kaimu Jaji Mkuu  wa  Tanzania,  Mhe. Profesa Ibrahim   Juma, amewataka  mawakili  kufanya kazi kwa kuangalia sheria za nchi  na za kimataifa ili kuweza kuwasaidia  Watanzania katika   masuala  yanayohusu sheria  hususan  wananchi wanyonge ili nchi iweze kufikia malengo ya kimaendeleo .

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Jaji Mkuu huyo, wakati wa hafla fupi ya 56 (1986-2017)  ya kuwakubali na kuwaapisha Mawakili wapya 248 iliyofanyika leo  kwenye Kiwanja cha Mahakama  Kuu kilichopo jijini Dar es Salaam.

“Leo tumewaapisha Mawakili  waliokubaliwa, nilifanya  nao mazungumzo kila mmoja, wengi wao ni vijana wadogo wenye miaka  25 hadi 30  ya  kufanya kazi ya sharia, hivyo  kukubaliwa kwao  sio mwisho wa kusoma wanapaswa  kusoma  sheria za kimataifa ili kufahamu  sheria za utaratibu wa nchi zingine,” alisisitiza . 

Profesa Juma aliwataka  Mawakili hao, waendelee kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia maadili  na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya rushwa,kwa sababu    bado wananchi  wana   hisia  kwamba  tatizo la rushwa  ni kubwa  ndani ya Mahakama  ya Tanzania.

"Wazazi  na Serikali imetumia  gharama  kubwa  kuwasomesha,  hivyo watambue  mchango huu,  waisaidie  Serikali  na wazazi wao ili  Tanzania  isonge mbele, alisisitiza.
Akijibu  swali lililoulizwa na  baadhi ya waandishi kuhusu kuwepo kwa tetesi kwamba  Chama cha Mawakili  Tanzania (TLS) kinaweza kufutwa,  Kaimu jaji Mkuu alisema sheria  ikitungwa haitalenga  mtu wala taasisi, hivyo  hofu hiyo haina sababu  kuwepo  kwa kuwa Mawakili ni sehemu ya Mahakama.


 
 
 
 
 
 
 
 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni