Jumatano, 28 Juni 2017

MKOA WA KIGOMA KUJENGEWA MAHAKAMA KUU HIVI KARIBUNI.

Na Magreth Kinabo

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinad Wambali  amesema kwamba mkoa wa Kigoma utapatiwa Mahakama  Kuu hivi karibuni,ikiwa ni hatua ya kuwaondolea  adha wanaoipata wananchi ya kutafuta huduma ya mahakama  hiyo kutoka eneo moja hadi jingine.
Kauli hiyo   imetolewa  mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Kiongozi wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama  ya  Wilaya  ya Kibondo kuhusu malengo ya ziara yake katika mkoa wa Kigoma, hivyo aliwataka  baadhi  ya viongozi  na  wananchi kuvuta subira.

Jaji Kiongozi , pia alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mahakama Kuu  Kanda  ya Tabora, wakiwemo baadhi ya watumishi wa Mahakama  Kuu kutoka  kanda hiyo  ambayo inajumuisha mikoa miwili yaani na Tabora na Kigoma.  

“Tayari kiwanja kimeshapatikana na eneo la Buhigwe  na tenda imeshatangazwa, hivyo mchakato wa ujenzi utaanza hivi, karibuni,”alisema Jaji Kiongozi.
 Kiwanja  hicho kina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 16,000. Mkoa  huo, unahitaji  huduma ya Mahakama Kuu  kwa sababu ya kukua kwa   idadi ya watu,pia hivi sasa watu wanatoka  katika mkoa  huo  kwenda kufuata  huduma za Mahakama Kuu mkoa wa Tabora , pia kukua  kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Jaji Kiongozi   aliongeza katika kanda hiyo, wilaya ambazo hazina   mahakama za wilaya zitajengewa mahakama kwa kuwa Mahakama  ya Tanzania kupitia mpango Mkakati wa Miaka Mitano(2015/16 hadi  2019/20 imejipanga kujenga mahakama kila wilaya, tarafa na kata.



Jaji Kiongozi Mahakama  Kuu ya Tanzania, Mhe, Ferdinand Wambali (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja  na  baadhi ya viongozi wa  Mahakama  Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Tabora  na Shinyanga  baada  kulitembelea  jengo la   Mahakama  Kuu Kanda ya Shinyanga  Juni,  26,mwaka huu, ambapo  alifanya ukaguzi  wa shughuli za utendaji kazi  na miundombinu ya Mahakama hiyo. Wengine ni  baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
 

Picha  ya muonekano  wa  jengo la  Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.


 


 

 









Hakuna maoni:

Chapisha Maoni