Alhamisi, 26 Oktoba 2017

HUKUMU YA KESI YA ELIZABETH MICHAEL KUTOLEWA NOVEMBA 13, MWAKA HUU


Msanii  maarufu nchini anayejulikana  kwa  jina maarufu  la ‘Lulu’ na jina lake halisi  Elizabeth  Michael   akiwa   katika Mahakama  Kuu ya Tanzania kwa ajili  kuendelea na kesi yake iliyopo katika Mahakama hiyo. Tukio hilo limetokea leo  asubuhi  jijini Dar es Salaam.



 Msanii  maarufu nchini anayejulikana  kwa  jina maarufu  la ‘Lulu’ na jina lake halisi  Elizabeth  Michael   akitoka  nje   ya  Mahakama  Kuu ya Tanzania baada ya   kesi yake inayomkabili   iliyopo katika Mahakama hiyo, kusikilizwa . Tukio hilo limetokea leo asubuhi  jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo ya msingi iliyoendelea  leo katika  Mahakama hiyo, ambapo  Wazeee wa Baraza la Ushauri walitoa majumuisho  ya ushahidi  wao,  kwa kudai  kuwa Elizabeth  aliaua  bila ya kukusudia.

Ambapo  Jaji wa  Mahakama  Kuu  ya   Tanzania , Mhe .  Mhe.  Sum  Rumanyika, ambaye   aliwataka  wazee hao, kutoa maoni  yao  kwa kuzingatia msingi  wa sheria . Pia  aliongeza  kwamba  yuko  tayari kuyapokea.

Kesi hiyo imeendeshwa  na mawakili  upande wa Serikali(Mashtaka)  umeongozwa  na  Faraja George na Upande wa Utetezi umeongozwa na Peter  Kibatala.

Aidha  Jaji  Rumanyika  baada ya kusikiliza  maelezo  hayo,  alisema  hukumu ya kesi hiyo, inatarajiwa  kutolewa   Novemba  13, mwaka huu.
(Habari  na Picha  Magreth  Kinabo  )

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni