Jumatano, 25 Oktoba 2017

MAJUMUISHO YA KESI YA MSANII ELIZABETH MICHAEL KUFANYIKA KESHO

Msanii  maarufu nchini anayejulikana  kwa  jina maarufu  la ‘Lulu’ na jina lake halisi  Elizabeth  Michael   akiwasili  katika Mahakama  Kuu ya Tanzania kwa ajili  kuendelea na kesi yake iliyopo katika Mahakama hiyo. Tukio hilo limetokea leo asubuhi  jijini Dar es Salaam.
Kesi  hiyo inayoendeshwa  na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.  Sam  Rumanyika. Katika  kesi hiyo  ya msingi  namba 125 ya mwaka  2012, inadaiwa  kuwa Aprili 2, mwaka 2012  kwenye  eneo la Vatican  jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua  Msanii  wa filamu , Steven  Kanumba  bila kukusudia. Kesi  hiyo  itaendelea kesho  tarehe 26.10.2017 kwa ajili ya majumuisho.

Msanii  maarufu nchini anayejulikana  kwa  jina maarufu  la ‘Lulu’ na jina lake halisi  Elizabeth  Michael   akiingia ndani  ya jengo  la   Mahakama  Kuu ya Tanzania kwa ajili  kuendelea na  utetezi  wa kesi inayomkabili   iliyopo katika Mahakama hiyo. Tukio hilo limetokea leo asubuhi  jijini Dar es Salaam.

Kesi  hiyo inayoendeshwa  na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.  Sam  Rumanyika. Katika  kesi hiyo  ya msingi  namba 125 ya mwaka  2012, inadaiwa  kuwa Aprili 2, mwaka 2012  kwenye  eneo la Vatican  jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua  Msanii  wa filamu , Steven  Kanumba  bila kukusudia. Kesi  hiyo  itaendelea kesho  tarehe 26.10.2017 kwa ajili ya majumuisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni