Jumanne, 12 Desemba 2017

MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA AFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI MKUU WA TANZANIA

Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipomtembelea ofisini kwake. 
Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik akiwa ofisini kwa Jaji. Katika mazungumzo hayo, Bw. Malik ameisifu kazi nzuri inayofanywa na Mahakama katika kuboresha huduma zake pamoja na kutekeleza Mpango Mkakati wa miaka Mitano (2015/16-2019/2020). Aidha Mtaalamu huyo amesisitiza juu ya umuhimu wa Mahakama kuwapatia Mafunzo watumishi wake hususan Tehama ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi. Bw. Malik pia imemshauri Mahakama kuboresha mfumo wa Mawasiliano hasa kwa upande wa utoaji wa habari kuhusu Maboresho kwa wananchi ili waweze kufahamu. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimsikiliza Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake. Mhe. Jaji Mkuu aliishukuru Benki ya Dunia kwa kufadhili Miradi ya Maboresho ya Mahakama. Alisema pamoja na kuendelea kwa kazi ya uboreshaji wa miundombinu hasa majengo Mahakama pia inaendelea na kazi ya kutoa Mafunzo kwa watumishi ili kuboresha huduma za Mahakama. 
 
 Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik akisisitiza jambo kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma. 



 Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Jaji Mkuu. 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka Benki ya Dunia Bw. Waleed Malik aliyemtembelea ofisini kwake. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Kattanga na wa pili kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama na Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama Mhe. Zahara Maruma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni