Jumanne, 30 Januari 2018

JAJI MKUU AZINDUA JENGO JIPYA LA MAHAKAMA YA WILAYA BAGAMOYO

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (pichani) (kulia) akikata utepe kuzindua rasmi jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo mapema Januari 30, 2018, anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo, jengo hilo la kisasa kabisa lilijengwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi  umegharimu jumla ya Tshs.591,837,919, aidha ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo ulienda sambasamba na ujenzi wa nyumba mbili (2) za Mahakimu zilizogharimu kiasi cha Tshs. 106, 568,514 na kufanya jumla ya kiasi cha 626,406,433 kwa majengo yote ie. Jengo la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo pamoja na nyumba mbili. Mhe. Jaji amesema lengo ni kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi ya utoaji haki nchini.
Mhe. Jaji Mkuu pamoja na Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa pamoja wakifurahi kwa pamoja mara baada ya Mhe. Jaji Mkuu kuzindua rasmi jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo.
Mhe. Jaji Mkuu pamoja na Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa pamoja wakifurahi kwa pamoja mara baada ya Mhe. Jaji Mkuu kuzindua rasmi jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo, jengo hili ni miongoni mwa majengo mapya yanayozinduliwa ndani ya Wiki ya Sheria iliyoanza rasmi Januari 27 hadi Januari 31, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa Mahakama mpya ya Wilaya Bagamoyo, ameipongeza Mahakama kwa kusogeza miundombinu ya Mahakama katika Mkoa huo.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama pamoja na wananchi mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo. 
Kikundi cha burudani ya ngoma (Tasuba) kikitoa burudani katika hafla hiyo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa hotuba katika uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo.
Ukaguzi wa jengo jipya, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, kushoto akieleza jambo mbele ya Mhe. Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama na Serikali  walipokuwa wakikagua jengo hilo la kisasa mara baada ya uzinduzi rasmi.
Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Pwani waliohudhuria katika hafla hiyo.  
Meza kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mahakama na Serikali mara baada ya kukamilika kwa hafla ya uzinduzi, aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.  Ibrahim Hamis Juma,  wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Eng. Evarist Ndikilo, wa pili kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa kwanza kulia ni Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi, waliosimama, mwenye tisheti nyekundu ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa tatu kulia ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, wa kwanza kushoto ni Mhe. Sollanus Nyimbi, Mtendaji-Mahakama ya Rufani  pamoja na Maafisa wengine Waandamizi wa Mahakama ya Tanzania.
Mgeni rasmi akipanda mti wa kumbukumbu katika jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo hilo.  
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akipanda mti wa kumbukumbu katika jengo la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo.
(Picha na Mary Gwera)
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni