Waheshimiwa Majaji
wapya wa Mahakama Kuu walioteuliwa kutoka Mahakama wakiwa katika picha ya
pamoja, katikati ni Mhe. Ilvin Mugeta, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kushoto
ni Mhe. Elinaza Luvanda, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na aliyesimama kulia
ni Mhe. Mustapher Siyani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Majaji hawa
wameagwa rasmi mapema Mei 04, 2018 na Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania.
Sehemu ya Wajumbe wa
Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakiwa katika kikao kilichofanyika katika
Ukumbi wa Maktaba-Mahakama ya Rufani, katika kikao hicho Wajumbe hao walipata
fursa ya kuwaaga waliokuwa Wajumbe wa Menejimenti ambao waliteuliwa hivi
karibuni kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, walioketi mbele (katikati) ni
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.
Hussein Kattanga, kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa kikao hicho ambaye pia ni
Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na kushoto ni
Msajili-Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza.
Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe
wa Menejimenti, katika salaam zake za shukrani, Mhe. Jaji Mugeta ameishukuru
Menejimenti kwa ushirikiano katika kipindi chote alichofanya kazi katika nafasi
ya Msajili-Mahakama Kuu, aidha; Mhe. Mugeta ameomba ushirikiano zaidi katika
nafasi hii mpya.
Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Elinaza Luvanda akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa
Menejimenti, amemshukuru Mhe. Rais na Viongozi wengine wa Mahakama kwa uteuzi
wa nafasi hiyo, na ameahidi kutoa ushirikiano katika kazi yake.
Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani akitoa salaam za shukrani kwa Wajumbe wa
Menejimenti, amewashukuru Wajumbe wote kwa kufanya kazi kwa ushirikiano,
vilevile amesisitiza kuendelea kujadili mambo ya msingi katika vikao hivyo
kwani Menejimenti ni moyo wa Mahakama ambayo inafanya kazi kubwa ya kusukuma
vitu kwenda mbele.
Mwenyekiti wa kikao cha
Menejimenti ya Mahakama ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.
Hussein Kattanga (kushoto) akikabidhi zawadi ya nakala za Vitabu vya Mpango
Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Ilvin Mugeta
(kulia), anayeshuhudia zoezi hilo (katikati) ni Msajili Mkuu- Mahakama ya
Tanzania, Mhe. Katarina Revocati.
Mwenyekiti wa kikao cha
Menejimenti ya Mahakama ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.
Hussein Kattanga (kushoto) akikabidhi zawadi ya nakala za Vitabu vya Mpango
Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya
Tanzania (2015/2016-2019/2020) kwa Mhe. Jaji Elinaza Luvanda (kulia)
anayeshuhudia ni Msajili Mkuu- Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati.
Mhe. Jaji Elinaza
Luvanda (kulia) akipeana mkono na Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. John
Kahyoza (kushoto) mara baada ya kupokea nakala zake za Mpango Mkakati wa
Mahakama ya Tanzania.
Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (kulia) akipokea nakala ya Kitabu cha Mpango
Mkakati kutoka kwa Mtandaji Mkuu Mahakama (kushoto).
Picha ya pamoja
Wahe. Majaji na Wajumbe
wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania, aliyeketi katikati ni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, wa pili kushoto ni Mhe. Elinaza
Luvanda, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Mhe. Mustapher
Siyani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa kwanza kulia ni Mtendaji
Mkuu-Mahakama ya Tanzania na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu-Mahakama ya
Tanzania.
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni