Alhamisi, 17 Januari 2019

WAJUMBE WA CHAMA CHA WANASHERIA CHA NCHINI CHINA WATEMBELEA MAHAKAMA YA TANZANIA


 Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (aliyesimama) akizungumza na Wageni kutoka Chama cha Wanasheria cha nchini China (CLS) wakati ujumbe huo ulipotembelea ofisini kwake kwa lengo la kujua mfumo mzima wa utendaji kazi wa Mahakama, vilevile  kuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya Kisheria, aliyeketi katikati ni Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Mhe. Jaji Dkt. Benhajj Shaaban  Masoud ambaye alimuwakilisha Mhe. Jaji Kiongozi katika mazungumzo hayo, kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria China, Bw. Wang Wei ambaye pia ni Kiongozi wa msafara huo akiwatambulisha Wajumbe alioambatana nao, aidha Bw. Wei alitumia fursa hiyo pia kuikaribisha Mahakama ya Tanzania kushiriki katika Semina na Makongamano mbalimbali yanayotarajia kufanyika nchini humo, mwaka huu.
 Sehemu ya Wageni hao kutoka Chama cha Wanasheria cha China wakiwa katika Mazungumzo.

Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Elizabeth Mkwizu akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya katika mazungumzo hayo.

Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama ya Tanzania (JDU), Mhe. Zahra Maruma akiwasilisha kwa wageni hao kuhusu maboresho mbalimbali na Mikakati iliyopo chini ya Mradi wa Maboresho wa huduma za Mahakama.
 Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania akimkabidhi zawadi za nakala za vijitabu vya Mpango Mkakati wa Mahakama pamoja na Majarida ya Mahakama kwa  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria China, Bw. Wang Wei.

Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania (kulia) akifurahia zawadi kutoka kwa Naibu Mkururgenzi Mkuu wa CLS, Bw. Wang Wei.

Mhe. Revocatti akiwaonesha wageni hao Ukumbi namba moja (1) wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni