Ijumaa, 18 Januari 2019

PROFESA KABUDI AITAKA TAASISI YA SLYNN KUTOA MAFUNZO YA MAKOSA JINAI


Na Magreth Kinabo

Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba leo amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Taasisi ya Slynn kutoka nchini Uingereza.
Mazungumzo hayo yamefanya katika ofisi ya Mahakama Kuu jiji Dar es Salaam, ambapo Waziri  huyo aliyataja maeneo ambayo yanahitaji ushirikiano wa mafunzo
mbalimbali, yakiwemo ya makosa ya jinai.

 “Tunahitaji  ushirikiano katika kuwajengea uwezo majaji na kubadilishana uzoefu, ikiwemo kubadilishana uzoefu katika masuala  ya kesi za jinai hususan zile zenye makosa makubwa na zenye  changamoto,” alisema Profesa Kabudi.

Profesa Kabudi aliongeza kwamba  mafunzo mengine ni katika maadili na ujuzi mbalimbali wa kisheria..

  Lengo la ujumbe huo, kutembelea Mahakama ya Tanzania ni pamoja na kujua taratibu mbalimbali za uendeshaji mashauri, kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi na vilevile kuona jinsi gani Taasisi inasaidia katika maeneo yatakayobainishwa,” alisema Bi. Fenney.

Taasisi ya Slynn iliyopo nchini Uingereza ina takribani umri wa miaka 30 inajihusisha na masuala ya haki na sheria na inafanya kazi  kwa karibu na Majaji na Taasisi za haki duniani ili kuboresha mifumo ya utoaji haki na uongozi wenye kufuata misingi ya sheria.

 Ujumbe huo ambao umefanya ziara ndani ya Mahakama kwa siku nne umejielekeza kujua zaidi jinsi gani Mahakama ya Tanzania inafanya katika suala zima la Usuluhishi ‘Mediation’ na masuala mengineyo.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi  akizungumza  leo na wajumbe kutoka  Taasisi ya Slynn.

mjumbe Sean Hichorst wa (pili kulia) akifafanua jambo  na (pili kulia)  ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Slynn , Alison Fenney. 

wajumbe kutoka Taasisi  Slynn Mhe. Lord Bonomy (wa kwanza kulia) na ( wa pili kulia )Nic Madge wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria , Profesa Palamagamba  Kabudi (hayupo pichani), alipokuwa anazungumza nao leo  kwenye ofisi ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati akizungumza leo kwenye mkutano wa Mazungumzo baina ya  na Waziri Katiba na Sheria  na ujumbe kutoka Taasisi ya Slynn   yaliyofanyika  kwenye ofisi ya  Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni