Jumanne, 5 Februari 2019

JAJI MKUU ATAKA USHIRIKIANO ZAIDI NA BENKI YA DUNIA


Na Mwandishi wetu-Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma ametaka ushirikiano mzuri uliopobaina ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia kuendelezwa.

Ameyasema hayo leo alipotembelewa na Timu ya Wataalamu kutoka Benki ya Dunia waliopo nchini kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa kwa ushirikiano na Benki hiyo.  


“Tunashukuru kwa namna ambavyo tumeweza kushirikiana kwa kiasi ambacho sasa tunaweza kuona mabadiliko, mathalani kupungua kwa malalamiko kutoka kwa wafungwa Magerezani”, amesema Jaji Mkuu.
 Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Kattanga amebainisha kuwa mradi wa maboresho unaotekelezwa na Mahakama ni wa aina yake kwa kuwa unahusu mabadiliko ya watu.  Mbali ya kushukuru kwa ushirikiano, amesisitiza kuwa Mahakama inafanya jitihada mbalimbali kutekeleza mipango yake kwa kuchukua mifano bora kutoka nchi za Ufaransa na Kazakhstan. 


Kwa upande wake Bw. Waleed Malik ameonyesha kuridhishwa kwake na kiwango cha maboresho kilichofikiwa katika Mahakama.
“Nimeridhishwa na kiwango na ubora wa huduma zinazotolewa kwenye maonesho na utoaji elimu kwa ujumla kule Dodoma.  Nimefurahia uratibu mzuri wa maadhimisho ya wiki ya sheria”, amesema Bw. Malik.  Ameongeza kuwa ameweza kubaini matokeo chanya na yanayoonekana.
Ujumbe wa Benki ya Dunia unaongozwa na Bi. Deborah Isser.  Wengine ni Bw. Waleed Malik na Bi. Clara Meghani. Katika ziara hiyo ujumbe huo utatembelea kanda za Mbeya, Mwanza, Mara na pia Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Lushoto.
Aidha, kikao hicho kilihudhuriwa pia na Jaji Kiongozi Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi; Msajili Mkuu wa Mahakama Mhe. Katarina Revocati; Mkuu wa Timu ya Maboresho ya Mahakama Bw. Solanus Nyimbi na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama Mhe. Zahra Maruma.  


Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma   (kushoto) akisalimiana na ni Mjumbe  kutoka Benki Deborah Isser baada ya kumtembelea ofisini, iliyoko Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma   (kushoto) akisalimiana na ni Mjumbe  kutoka Benki  ya Dunia Clara Maghani baada ya kumtembelea ofisini, iliyoko Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam.


Mjumbe  kutoka  Benki  ya Dunia Waleed Malik akisalimiana  na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma , wakati ujumbe kutoka Benki ya hiyo  ulipotembelea ofisi ya  Jaji Mkuu huyo , iliyopo  Mahakama ya Rufaa.

 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maboresho ya  Mahakama ya Tanzania Mhe.Zahra  Maruma akitoa neno la kuwakaribisha wajumbe kutoka  Benki  ya Dunia mara baada ya kutembelea ofisi ya  Jaji Mkuu, iliyopo  Mahakama ya Rufaa.
 Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma   akizungumza na wajumbe  kutoka Benki  ya Dunia baada ya kumtembelea ofisini , iliyoko Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam
Mjumbe  kutoka Benki  ya Dunia , Deborah Isser (wa kwanza kulia)akizungumza  jambo wakati ujumbe kutoka Benki ya hiyo  ulipotembelea ofisi ya  Jaji Mkuu, iliyopo  Mahakama ya Rufaa.



Picha ya pamoja kati ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma  (Katikati)(wa tatu kushoto) Deborah  Isser wa Pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga na wa kwanza kushoto ni Waleed Malik. Kulia  wa tatu ni Clara Maghani (wa pili kulia) ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe. Eliezer Feleshi na watatu kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni