Jumatatu, 4 Februari 2019

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, BENKI YA DUNIA WATEMBELEA MAONESHO WIKI YA SHERIA

 Waziri wa Katiba  Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimsikiliza Hakimu Mkazi Mwandamizi Mhe. Victoria Nongwa alipotembelea banda la Usimamizi wa Mashauri katika Maonesho ya wiki ya Sheria jijini Dodoma.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimsikiliza Mchumi wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Geofrey Mashafi  alipotembelea banda la Maboresho ya Mahakama katika Maonesho ya wiki ya Sheria jijini Dodoma.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na wananchi waliofika kwenye Maonesho kupata huduma na 
elimu ya sheria.
  
  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kondoa Mhe. Francis Mhina akisalimiana na Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia alipotembelea Maonesho ya wiki ya Sheria.


 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akielezea jambo kwa wataalamu kutoka Benki ya Dunia walipotembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma. Katikati ni Mtaalamu wa Benki ya Dunia 
Bwn. Walid Malik.

 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akielezea kuhusu ujenzi wa majengo ya Mahakama unaoendelea nchini. 
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga akielezea kuhusu ushikiano kati ya Mahakama pamoja na vyuo na shule za sekondari unaolenga kuwalea wanafunzi kuwa na Maadili mema katika jamii na baadaye kuwa watumishi wenye Maadili ndani ya Mahakama na sekta ya Sheria kwa ujumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni