Alhamisi, 7 Februari 2019

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AZINDUA MAHAKAMA
Na Magreth Kinabo

Waziri wa Katiba na sheria, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi  amewataka watumishi wa Mahakama  ya Wilaya ya Ilala iliyoko  Kinyerezi Jiji Dar es Salaama  kutoa huduma za utoaji haki bila ubaguzi, rushwa na weledi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri huyo wakati akizindua, Mahakama hiyo, ambapo alisema  imejengwa kwa ajili ya kusogeza huduma karibu na wananchi. Hivyo wananchi wanapaswa kupatiwa huduma  wanayostahili.

“Mahakama hii imengwa kwa ubora na ubunifu na wapongeza kwa kusogeza huduma  karibu na wananchi. Ninatoa wito tusiyachafue majengo ya Mahakama hii na kutoharibu miundombinu yake, bali kuyatunza,” alisema Profesa Kabudi.

Aliongeza kwamba Serikali inatambua miundombinu ya mahakama iliyopo, itaendelea kutenga bajeti  kwaajili ya kuiboresha.

Kwa upande wake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe .Eliezer Feleshi  aliwataka watumishi hao ,kufanya kazi kwa kujituma.

Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi akizundua Mahakama ya  Wilaya ya Ilala iliyoko Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni