Alhamisi, 26 Septemba 2019

MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA AKAGUA MIRADI YA UJENZI -MAHAKAMA LINDI

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga(wa pili kulia) akimweleza jambo Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Bw. Joseph  Chota wa (kwanza kulia).Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga alifanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa mahakama mnamo Septemba 23 na 24, mwaka huu ambapo alikagua kiwanja hicho, zikiwemo Mahakama mbili za Wilaya, ambazo ni  Mahakama ya Wilaya ya  Kilwa na Mahakama ya Wilaya ya  Ruangwa ili kuangalia hatua iliyofikiwa .
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga ( wa kwanza ) na kulia ni Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu  Mkazi Lindi , Mhe. James Karayemaha na kushoto (aliyevaa kofia) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha, wakikagua kiwanja cha ambacho kinatarajiwa kujengwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (aliyenyoosha mkono) akiwa na wahandisi, wakiwemo viongozi wengine wakikagua ramani ya kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.
Kattanga kulia) akisaini kitabu cha wageni katika  kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi. Kushoto ni Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu   Mkazi Lindi, Mhe. James Karayemaha.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga(kulia) akikagua ramani ya Mahakama ya Wilaya Kilwa.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (katikati) akikagua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kilwa.
Muonekano wa mbele wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kilwa.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kulia) akielezea jambo wakati akikagua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kilwa.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kulia) akikagua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kilwa .

(Picha na Hillary Rory – Lindi)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni