Jumanne, 10 Septemba 2019

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA HUDUMA ZA KIMAHAKAMA NA MAHAKAMA INAYOTEMBEA

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kimara, Mhe.Geiza (katikati) Mbeyu akiendelea na kazi ndani ya Mahakama Inayotembea katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo, iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam.

Gari ya Mahakama Inayotembea likiwa katika maeneo ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo, iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam likiendelea kutoa huduma za kimahakama.
Karani wa Mahakama ya Mwanzo, Kimara, Judith Mwakyalabwe, akiendelea na utendaji kazi ndani ya Mahakama Inayotembea wakati Mahakama hiyo ikitoa huduma eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kimara, Mhe. Geiza Mbeyu, akimsikiliza kwa makini mwananchi ambaye alikuwa akiuliza jambo kuhusu Mahakama Inayotembea katika eneo la Stendi ya Kibamba iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwananchi, Zubeda Abdallah Kombo akielekezwa na Karani wa Mahakama ya Mwanzo, Kimara,Judith Mwakyalabwe jinsi ya kupata hati ya kiapo.

(Picha na Aziza Muhali SJMC )

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni