Jumanne, 18 Februari 2020

UTENDAJI KAZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAMFURAHISHA JAJI MKUU -ETHIOPIA



Na Magreth Kinabo na Tawani Salum- Mahakama

Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Meaza Mengistu amefurahishwa na utendaji kazi  wa uwazi wa Mahakama ya Tanzania, ikiwemo huduma ya Mahakama inayotembea  (Mobile Court) kwa kuwa hurahisisha hutoaji haki kwa wakati.

Mhe. Mengistu alitoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea Mahakama inayotembea iliyokuwa ikitoa huduma kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, eneo Luguruni Mbezi na Mahakama ya Wilaya Kigamboni zilizopo jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Ethiopia alifurahishwa na Mahakama Inayotembea kwa jinsi inavyofanya kazi na kusema kuwa inasaidia  kuondoa mlundikano wa mashauri, pia husaidia kutoa huduma za kimahakama sehemu ambazo hazina mahakama, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu.

‘‘Mahakama hii ni suluhisho tosha la umalizwaji wa mashauri ndani ya Mahakama’’ pia vifaa vilivyopo ndani kwa mfano kuwepo kifaa maalum cha kuwapandishia walemavu, Mahakama hii imezingatia wenzetu walemavu na kuwa ni ishara tosha kuwa sasa Mahakama imedhamiria kuwa karibu na wananchi,” alisema Jaji Mkuu huyo.

Aliongeza kuwa aliamua kufanya ziara hapa nchini Tanzania baada ya kuona kuwa Mahakama ya Tanzania ina maboresho makubwa hivyo basi hakuweza kujiuliza mara mbili kuja kutembelea Mahakama ya Tanzania hasa kutokana na kasi ya umalizwaji wa mashauri, ujengwaji wa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo husaidia   kumalizwaji wa mashauri kwa wakati.

“Nimefurahishwa na maboresho makubwa ya ujenzi wa mahakama kwa kutumia teknolojia ya moladi yenye gharama nafuu na uwepo wa mazingira rafiki, ukiwemo utendaji kazi wa uwazi’’ alisisitiza.

Naye Mhe. Moses Ndelwa ambaye ni Mratibu wa Mahakama Inayotembea, alisema Mahakama hiyo, imeendelea kusikiliza mashauri kwa ngazi ya Mahakama ya Mwanzo. Hivyo kwa upande wa jiji la Mwanza mashauri 57 yalifunguliwa na kutolewa uamuzi.

Aliongeza kwamba katika jiji la Dar es Salaam mashauri 92 yalifunguliwa na kusikilizwa.  Pia mashauri yote yamesikilizwa na kutolewa uamuzi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

“Kwa mwananchi anayehitaji kufungua shauri la madai, anaweza kufungua katika Mahakama Inayotembea kama madai yake yanathamani isiyozidi shilingi  milioni hamsini (Tzs. 50,000,000/=). Mashauri yanaweza kufunguliwa moja kwa moja katika gari la Mahakama Inayotembea au katika Mahakama ya Mwanzo inayopatikana karibu na kituo ambacho Mahakama Inayotembea inatoa huduma.

Ndelwa alifafanua kuwa imekuwa ikisikiliza mashauri ya jinai yanayotokana na operesheni maalumu, ambapo jumla ya watuhumiwa 184 walifikishwa katika Mahakama inayotembea, mashauri yalisikilizwa ndani ya siku moja na kutolewa uamuazi.

Alisema mbali na usikilizaji wa mashauri, Mahakama hiyo inatoa huduma nyingine kama vile kutoa fomu za kiapo, kuthibitisha nyaraka mbalimbali, kutoa fomu za kufungulia mashauri, kutoa nakala za hukumu, kupokea malalamiko na kutoa vipeperushi pamoja na taarifa mbalimbali zinazohusu Mahakama.

Mpaka sasa takribani wananchi 97 wamepata huduma mbalimbali za kimahakama kupitia Mahakama Inayotembea.

Kwa upande wa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Agnes Mchome alisema  Mahakama hiyo katika kipindi cha mwaka 2019 mashauri yaliyofunguliwa ni 318, yaliyotolewa uamuzi 250 na yaliyobakia ni 186.

Wakati huohuo, Jaji Mkuu huyo alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) ambacho pia kinachohusisha Mahakimu na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wao.
Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (kushoto) akizugumza  leo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ,  Kisare Makori baada ya kufika katika ofisi hiyo   iliyoko Mbezi Luguruni,  jijini Dar es Salaami kwa ajili ya kujifunza kuhusu Mahakama Inayotembea inavyofanya kazi.

Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (kushoto) akipokewa  leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mejimenti ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania,  Mhe. Victoria Nongwa mara baada ya kuwasili katika  ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo iliyoko Mbezi Luguruni, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza kuhusu Mahakama Inayotembea inayofanya kazi, ambapo alifurahishwa na husogezaji wa huduma za mahakama kwa wananchi.



Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (mwenye kitenge) akitoka katika  ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubugo iliyoko Mbezi Luguruni, jijini Dar es Salaam wengine ni baadhi ya watalaamu kutoka Benki ya Dunia na Viongozi wa Mahakama ya Tanzania.



Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (kushoto) akipata maelezo leo kuhusu  gari maalum la Mahakama Inayotembea  linavyofanyakazi kutoka kwa  na Kaimu Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania,  Mhe. Victoria Nongwa mara baada ya kuwasili katika  ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo iliyoko Mbezi Luguruni, jijini Dar es Salaam.


Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (kushoto) akiuliza jambo  leo baada kujifunza kuhusu Mahakama Inayotembea  inavyofanya kazi  na kuhifurahia huduma hiyo   mara baada ya kuwasili katika  ofisi ya Mkuu wa  ya Ubungo iliyoko Mbezi Luguruni, jijini Dar es Salaam.



Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (katikati) akisikiliza jambo  leo kuhusu Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) unavyofanya kazi katika gari maalum la Mahakama Inayotembea kutoka kwa Mkurugenzi wa  TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania,  Bw. Kalege Enock (kulia) mara baada ya kuwasili katika  ofisi ya Mkuu wa  ya Ubungo iliyoko Mbezi Luguruni, jijini Dar es Salaam, ambapo gari hilo lilipokuwa likitoa huduma. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Mahakama Kuu ya Ethiopia, ambaye aliambatana na mgeni huyo, Mhe. Tesfaye Niwai.

Picha ya pamoja ya kati ya  Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (aliyevaa kitenge)  na baadhi ya wataalam kutoka Benki ya Dunia na Viongozi  na watumishi wa Mahakama ya Tanzania baada ya kutembelea huduma  ya gari maalum la Mahakama Inayotembea, iliyokuwa ikitolewa  leo kwenye eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,  jijini Dar es Salaam.



Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (aliyevaa kitenge)   akipokewa na  Hakimu Mkazi  Mfawidhi  Mwandamizi, Mhe.  Agnes Mchome wa Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, baada ya kuwasili leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni na Mahakama ya Mwanzo Kigamboni iliyopo  jijini Dar es Salaam. (aliyevaa gauni jeusi) ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt. na mwenye tai nyekundu ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Bw. Wleed Malik.
Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (kushoto) akitembelea   Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni iliyopo jijini Dar es Salaam, ambapo alijifunza kuhusu ujenzi wa Mahakama hiyo kwa kutumia gharama nafuu na yenye mazingira rafiki. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra  Maruma  na  wa kwanza ni Hakimu Mkazi  Mfawidhi  Mwandamizi, Mhe.  Agnes Mchome  wa Mahakama  ya Wilaya ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.


Hakimu Mkazi  Mfawidhi  Mwandamizi, Mhe.  Agnes Mchome  wa Mahakama  ya Wilaya ya  Kigmboni, jijini Dar es Salaam,  akitoa taarifa  ya kuhusu utendaji kazi wa mahakama hiyo,  kwa Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (ambaye hayupo pichani) .
 Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu  (aliyevaa kitenge) akiwa  katika picha ya pamoja)  na baadhi ya Viongozi wa  Mahakama ya  Tanzania wakati alipotembelea leo Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni iliyopo jijini Dar es Salaam, ambapo alijifunza kuhusu ujenzi wa Mahakama hiyo kwa kutumia gharama nafuu na yenye mazingira rafiki. (Kulia wa kwanza) ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra  Maruma, wa pili kulia ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik, wa tatu kulia ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Bi Clara Maghani. (aliyevaa shati la bluuni) ni   Makamu wa Rais wa Mahakama Kuu ya Ethiopia, ambaye aliambatana na mgeni huyo, Mhe. Tesfaye Niwai, (wa kwanza kushoto) ni Hakimu Mkazi  Mfawidhi  Mwandamizi, Mhe.  Agnes Mchome  wa Mahakama  ya Wilaya ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.



Jaji Mkuu huyo(aliyevaa kitenge) akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) ambacho pia kinachohusisha Mahakimu  wakati aalipowatembelea leo kwa ajili  ya kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wao kwenye  Mahakama Kuu ya Tanzania.
Jaji Mkuu wa Ethiopia, Mhe.  Meaza Mengistu (kushoto) akizungumza jambo na wanachama wa TAWJA na kulia ni Mwenyekiti wa TAWJA, ambaye pia ni  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De. Mello.

(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni