Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi ameendelea na ziara yake katika Kanda ya Mwanza ambapo jana alikagua shughuli za Mahakama katika wilaya ya Ukerewe. Pichani akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Ukerewe. Kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika.
Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Ukerewe wakimsikiliza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi alipokuwa akizungumza nao. Amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu na kuw na utayari wa kujiendeleza kitaaluma. Jaji Kiongozi pia amesisitiza umuhimu wa matumizi ya Tehama katika kazi za Mahakama.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza alipokuwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Cornel Magembe alipomtembelea jana.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Cornel Magembe (wa pili kushoto) pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo na Watumishi wa Mahakama.
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Cornel Magembe akimsikiliza Jaji Kiongozi alipomtembelea ofisini kwake jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni