Jumanne, 22 Desemba 2020

SIMAMIENI MABORESHO NA UWEKEZAJI UNAOFANYWA NA MAHAKAMA – JAJI MKUU

 Na Innocent Kansha

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakabidhi Mahakimu Wakazi Wafawidhi wawili wa mikoa ya Geita na Iringa Hati au nyenzo za kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya Uhakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Hati iliyofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo Desemba 22, 2020 Jaji Mkuu amewataka Mahakimu hao kwenda kusimamia utendaji wa kazi za Mahakama za kila siku na nidhamu za watumishi katika maeneo yao ya kiutawala.

“Mmeaminiwa na utawala, nataka mkawe mfano kwenye suala la usimamizi wa maboresho na uwekezaji mkubwa wa mifumo yetu ya Teknologia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mikoa yenu”, alisema Mhe. Jaji Prof. Juma.

Mahakama imefanya uwekezaji mkubwa na maboresho mbalimbali katika nyanja ya TEHAMA, imeweka mifumo mingi ya kusaidia kurahisisha utoaji haki, kama vile Mfumo wa uhuishaji na kusajili mashauri Mahakamani JSDS II, Mahakama Mtandao maarufu kama “Video Conference”, Kusajili mashauri kwa njia ya mtandao “E – Failing” na mfumo wa kutambua Mahakama “Judicial Maping”.

Aidha, Mhe. Jaji Mkuu aliwasisitiza kusimamia kwa karibu matumizi ya mifumo hiyo ili iweze kuleta matokeo chanja katika utendaji kazi.  

Mhe. Jaji Mkuu alisema bado kuna changamoto mbalimbali katika suala la uchakataji wa takwimu sahihi za mashauri kupitia mfumo wa JSDS II, pia bado wadau wanasajili mashauri kwa njia ya kawaida mahakamani, tilieni mkazo kwenye maeneo hayo ili maboresho haya yalete maana katika utendaji wa kazi.  

Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa hati kulia ni Mhe. Said Ally Mkasiwa ambaye amekabidhiwa hati ya kwenda kuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, kushoto ni Mhe. Cleofas Frank Waane ambaye pia amekabidhiwa hati ya kwenda kuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita wakiwa katika picha ya pamoja

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma akisaini hati ya kuwakabidhi Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya. Hafla hiyo limefanyika leo  Desemba 22, 2020 katika Ofisi yake Jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma akimkabidhi Hati Mhe. Said Ally Mkasiwa kwenda kuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma, (wa pili kushoto) akiwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi wakiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi  Wafawidhi katika hafla ya kuwakabidhi Hati.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma (watatu kushoto), Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa tatu kulia), Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma (wa kwanza kushoto), Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Kevin Mhina (wa pili kulia), Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Sharmillah Sarwatt (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi Wafawidhi mara baada ya kukabidhiwa hati.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma (aliyesimama) akitoa muongozo wa namna ya kukabidhi Hati kwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya wakati wa hafla, kulia ni Jaji  wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, wa pili kushoto ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina na wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Bw. Leonard Magacha

  

 (Picha na  Innocent Kansha – Mahakama)

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni