Jumatano, 23 Desemba 2020

RAIS AMTEUA JAJI MWANGESI KUWA KAMISHNA WA MAADILI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, uteuzi wa Jaji Mwangesi unaanza rasmi leo Desemba 23, 2020 na ataapishwa kesho tarehe 24 Disemba, 2020 saa 4:00 Asubuhi Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

Mhe Mwangezi ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela kufariki dunia.

MAHAKAMA YA TANZANIA INAMPONGEZA JAJI MWANGESI KUFUATIA UTEUZI HUO.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni