Ijumaa, 26 Februari 2021

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE. SAMWEL KARUA AMEFARIKI DUNIA

 

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Samwel Karua amefariki dunia leo Februari 26 katika hospitali ya Seifi iliyopo Oystebay jijini Dar es salaam. 

Msiba upo nyumbani kwake Kijitonyama na mipango ya mazishi itajulikana hapo baadaye.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 


Maoni 1 :