Jumapili, 5 Septemba 2021

MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA AKAGUA UKARABATI WA JENGO LA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOSHI

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel alifanya ziara ya kikazi Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya watumishi wa kanda hiyo.

Prof. Ole Gabriel amewataka watumishi wa kanda hiyo kuzingatia mambo matano muhimu wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. 

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kutobaguana kwa namna yoyote, kutojihusisha na vitendo vya rushwa, uvivu na uzembe na kutochelewesha mashauri mahakamani pasipokuwa na sababu za msingi.

Aidha, Mtendaji Mkuu wa Mahakama alitembelea na kukagua kazi ya ukarabati wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi. 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akisoma ramani ya Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi alipokwenda kukagua kazi ya ukarabati wa jengo hilo inayoendelea.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kwa lengo la  kukagua kazi ya ukarabati inayoendelea.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akishuka ngazi baada ya kumaliza kukagua kazi ya ukarabati inayoendelea kwenye jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi Bw. Donald Makawia akimuelezea jambo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akikagua kazi ya ukarabati inayoendelea kwenye jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi ambalo hivi sasa linafanyiwa ukarabati ili kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akipanda Mti wa kumbukumbu ya kutembelea na kukagua ukarabati wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel mara baada ya kupanda Mti wa kumbukumbu ya kutembelea na kukagua ukarabati wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi baada ya kuzungumza nao.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza nao.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi Bw. Donald Makawia akisoma Taarifa ya Utekelezaji wakati wa ziara ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni