Jumanne, 28 Mei 2024

MAFUNZO AWAMU YA NNE YA PROGRAM MAALUMU YA USHAURI KITAALUMA YAFANYIKA DODOMA

Na Arapha Rusheke-Mahakama Kuu Dodoma 

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo, kwa niaba ya Jaji Kiongozi, jana tarehe 27 Mei, 2024 alifungua mafunzo awamu ya nne ya program maalumu ya ushauri wa kitaaluma (Mentorship Programme) kwa Majaji, Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi wa ngazi mbalimbali.

 

Mafunzo hayo ya siku tatu inayofanyika katika Hoteli ya Vizano jijini hapa imeandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania kwa ufadhili wa Programu ya Kujenga Mfumo Endelevu wa Mapambano dhidi ya Rushwa Nchini Tanzania (BSAAT)

 

Mhe. Massabo alitoa shukrani za pekee kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma sio tu kwa kukubali mafunzo hayo kufanyika lakini pia kwa kuwaruhusu maafisa wote wa Mahakama waliohudhuria kushiriki kikamilifu.

Kadhalika, Jaji Mfawidhi aliwapongeza Hakimu Mkazi Mkuu, Mhe. Richard Kabate na Afisa Utumishi, Bw. Nkuruma Katagira kwa kazi nzuri waliyofanya ya kufuatilia mradi huo mpaka ukakaa sawa na kuhakikisha fedha zinapatikana. Aliwasihi washiriki wajifunze kwa umakini na weredi ili wakirudi vituoni mwao wawe sehemu ya kuboresha utendaji kazi.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dodoma, Mhe. Edwin Kakolaki, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Songea, Mhe. James Karayemaha na Mkurugenzi Huduma Saidizi – Hospital ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dkt Godwin Mwisomba.

Hii ni mara ya kwanza program hiyo kufanyika mkoani Dodoma. Awamu ya kwanza hadi ya tatu zilifanyika Mkoa wa Arusha. Lakini pia 

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Maafisa wa Mahakama katika uendeshaji wa mashauri ya rushwa na uhalifu mkubwa wa kupangwa (Corruption and Organised Crime Cases).

Mafunzo hayo pia yanalenga kukuza uelewa, ujuzi na ufanisi kwa washiriki katika kuhusiano wa kitaalamu miongoni mwao, kujenga kada ya washauri bora, kubaini na kuboresha mbinu za uendeshaji wa mashauri na uongozi.

Ufunguzi wa mafunzo hayo ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Mahakama Dodoma, akiwemo Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Silivia Lushasi, Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu Dodoma, Bi. Arapha Rusheke na Msaidizi wa Sheria wa Jaji, Mhe. Getrude Missana.

Meza kuu akiwemo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo (katikati). Kulia kwake ni Hakimu Mkazi Mkuu, Mhe. Richard Kabate na kushoto kwake ni Mhadhiri Chuo cha Uongozi Lushoto(IJA), Bi Fatma Mgomba. 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo akisoma hutuba ya ufunguzi kwa niaba ya Jaji Kiongozi katika ukumbi wa mkutano uliopo Vizano Hoteli Jijini Dodoma.

Hakimu Mkazi Mkuu, Mhe. Richard Kabate akiongea neno wakati wa mafunzo hayo.



Mhadhiri Chuo cha Uongozi Lushoto (IJA), Bi. Fatma Mgomba (aliyesimama) akiongea neno la utambulisho kwa washiriki wa program hiyo katika ukumbi wa mkutano uliopo Vizano Hoteli Jijini Dodoma.

Meza kuu inayoongzwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo (katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawezeshaji wa mafunzo hayo.

Meza kuu inayoongzwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo (katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu.

Meza kuu inayoongzwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo (katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Naibu Wsajili waliohudhuria mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mafunzo hayo.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni