Na Magreth Kinabo- Mahakama
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi amesema marehemu Jaji mstaafu wa Mahakama wa Kuu, Juxon Mlay alikuwa ni mtu wa haki na maamuzi yake yameacha alama katika sekta ya sheria.
Mhe. Jaji Maghimbi alisema kwa niaba ya, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani kwenye Ibada ya kuuga mwili wa marehemu Jaji Mlay iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Azania Front, lililoko jijini Dar es Salaam.
“Jaji Mlay hakupenda chombo chochote kujibebesha mamlaka, ambayo hakijapewa, hivyo alikuwa ni mtu wa haki ambaye anasisitiza kwa kuzingatia sheria,”alisema Mhe. Jaji Maghimbi.
Aliongeza kwamba atakumbukwa kwa maamuzi na miongozo aliyoamua kwa kuwa yataendelea kutumiwa na yameacha alama ambayo haitasahulika.
Jaji Maghimbi alisema marehemu alikuwa akipenda kuona amri zinazotolewa na Mahakama zinatekelezwa ipasavyo.
Naye Kiongozi wa Ibada hiyo,ambaye ni Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo, Chediel Lwiza alisema marehemu alikuwa ni mcha mungu, huku akisisitiza kwamba kazi ya ujaji, uhakimu na uwakili ni ya mungu na mungu ni wa haki, hivyo ili kuweza kutimiza wajibu katika kutoa haki ni lazima na mahusiano na mungu.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mahakamu Kuu,wakiwemo majaji wastaafu, viongozi wa serikali wastaafu na waombelezaji mbalimbali.
Marehemu Jaji Mlay alifariki dunia tarehe 25 Mei, 2024, mwili wake utasafirishwa kesho mkoani Kilimanjaro na utazikwa Ijumaa tarehe 31Mei, 2024 nyumbani kwake Himo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi akizungumza wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa Jaji mstaafu wa Mahakama wa Kuu, marehemu Juxon Mlay , iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Azania lililoko jijini Dar es Salaam.
Waombelezaji wakiwa katika ibada.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe Angela Bahati akimpa pole mke marehemu Flora Mlay (aliyevaa mewani).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni