- Yaahidi kulichakaza Bunge
Na ARAPHA RUSHEKE NA JEREMIA LUBANGO - Mahakama, Dodoma
Timu ya Mahakama inayoundwa na Majaji, Naibu Wasajili na Mahakimu imefanya mazoezi yake ya mwisho katika viwanja vya Shule ya St. Gasper Jijini Dodoma leo tarehe 21 Juni, 2024 kujiweka sawa na Bonanza la kimichezo lililoandaliwa na Bunge (Bunge Gland Bonanza).
Bonanza hilo litatimua vumbi kesho tarehe 22 Juni, 2024 katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.Mazoezi hayo yameongozwa na Kocha Spear Mbwembwe aliyekuwa Mchezaji wa Simba Sport Clubmwaka 1990-91.
Akizungumza katika viwanja hivyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma,Mhe. Fahamu Hamidu Mtulya, ambaye pia ni mmoja ya wachezaji wa timu hiyo, amewaomba Wadau na Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Bonanza hilo.
Mhe. Mtulya ametumia fursa hiyo kulipongeza Bunge kwa kuialika Mahakama katika Bonanza hilo, kwani kitu hicho hakikuwahi kutokea huko nyuma. Alisema kuwa Majaji wa Mahakama ya Tanzania nao ni Wanamichezo.
“Kesho asubuhi kwenye Uwanja wa Jamuhuri hapa Dodoma mtajionea Majaji wakisaidiwa na Naibu Wasajili wanavyotandaza kabumbu la 3-5-2 wakiifunga timu ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mhe. Mtulya.
Naye Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) Mhe, John Kahyoza, ambae ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Manyara, amesema Bonanza hilo ambalo limejumuisha Mihimili mbalimbali, ikiwemo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni fursa ya pekee ya kufahamiana na kujenga umoja na kuamusha hamu ya kufanya mazoezi na maendeleo ya kujenga afya.
Alisema timu yake inashirikisha Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu na Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu.
“Bonanza hili ni kubwa sana, liajumuisha Taasisi, Mihimili na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lengolikiwa kushiriki mazoezi kwa maendeleo ya Taifa na ni jambo jema na kubwa,” alisema Mhe.Kahyoza.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni