Jumanne, 23 Julai 2024

TANZIA - MTUMISHI WA MAHAKAMA YA WILAYA MBARALI MBEYA AFARIKI DUNIA


Marehemu Lucia Mwakalonge enzi za uhai wake.

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bi. Lucia Mwakalonge aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Wilaya Mbarali mkoani Mbeya kwa Cheo cha Mwandishi Mwendesha Ofisi.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Bi. Mavis Miti marehemu Lucia amekutwa na umauti  leo tarehe 23 Julai, 2024 majira ya mchana alipokuwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya 'Ocean Road' jijini Dar es Salaam.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa baada ya mipango ya mazishi kukamilika.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba wa mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni