Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Bw. Deogratias Raphael Rutainurwa aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Wilaya Muleba iliyopo Mkoa wa Kagera kwa nafasi ya Mlinzi Mwandamizi.
Kwa mujibu wa Afisa Tawala wa Mahakama ya Wilaya Muleba, Bi. Edventina Semba amesema Bw. Rutainurwa alifikwa na umauti tarehe 12 Julai, 2024 wakati akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bukoba.
Bi. Semba amesema kwa sasa msiba upo nyumbani kwake kijiji cha Makarwe Muleba na maziko yatafanyika leo tarehe 15 Julai, 2024.
Mahakama ya Tanzania inaungana na
ndugu, Jamaa na Marafiki kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na mpendwa
wetu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
AMEN.
Bw. Deogratias Raphael Rutainurwa enzi za uhai wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni