Mada mbalimbali zinaendelea kutolewa katika kikao kazi cha Mafunzo ya kujengeana na kubadilishana uzoefu kilichojumuisha ujumbe huo kutoka Mahakama ya Malawi na wenyeji wao kutoka Mahakama ya Tanzania kilichoanza tarehe 19 Agosti, 2024.
Mpaka sasa mada kadhaa zimetolewa ikiwa ni pamoja na Mfumo wa Utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania, Matumizi ya TEHAMA, Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala na nyingine.
Katika mawasilisho hayo yaliyotolewa na Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Mahakama wamewaeleza wageni hao kutoka kuwa, ili kuwa na maboresho ni muhimu kuwa na mipango thabiti, kubadili fikra na kuwa na Uongozi imara utakaounga mkono na kuwezesha kufikia azma hiyo.
Yafuatayo ni matukio katika picha ya kikao kazi cha Mafunzo ya kujengeana na kubadilishana uzoefu kilichojumuisha ujumbe huo kutoka Mahakama ya Malawi na wenyeji wao kutoka Mahakama ya Tanzania kinachoendelea kufanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Viongozi na Maafisa Waandamizi kutoka Mahakama ya Juu ya Malawi wakifuatilia mada inayotolewa katika ukumbi wa Hoteli ya Vizano jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick akiwasilisha mada kuhusu utendaji kazi wa Kurugenzi hiyo mbele ya ujumbe kutoka Mahakama ya Juu ya Malawi (hawapo katika picha).
Sehemu ya Viongozi na Maafisa Waandamizi kutoka Mahakama ya Juu ya Malawi na Mahakama ya Tanzania wakifuatilia mada inayotolewa katika ukumbi wa Hoteli ya Vizano jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Juu ya Malawi, Bi. Edith Chikagwa akizungumza jambo wakati wa kikao kazi cha Mafunzo ya kubadilishana uzoefu kinachoendelea kufanyika katika Hoteli ya Vizano jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hawa Mnguruta akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa mashauri ya mfumo wa utendaji kazi wa Mahakama nchini. Sehemu ya Watumishi kutoka Mahakama ya Tanzania wakiwemo Wakurugenzi Wasaidizi, Wakuu wa Vitengo na Maafisa wakifuatilia majadiliano yanayoendelea.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Fedha Mahakama ya Tanzania, Bw. Joseph Elikana akiwasilisha mada mbele ya ujumbe kutoka Mahakama ya Juu ya Malawi (hawapo katika picha).Sehemu ya Maafisa kutoka Mahakama ya Juu ya Malawi wakifuatilia kwa makini mada inayotolewa.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Kalege Enock akiwasilisha mada ya safari/maendeleo ya Mahakama kuhusu matumizi ya Teknolojia katika shughuli za utoaji haki nchini.Mkurugenzi wa Usimamizi wa Majengo na Uendelezaji wa Majengo la Mahakama ya Tanzania, Bw. Moses Lwiva akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Mafunzo ya kujengeana na kubadilishana uzoefu kilichojumuisha ujumbe huo kutoka Mahakama ya Malawi na wenyeji wao kutoka Mahakama ya Tanzania. Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso akiwasilisha mada leo tarehe 21 Agosti, 2024 katika kikao kazi cha mafunzo ya kujengeana na kubadilishana uzoefu kinachojumuisha ujumbe huo kutoka Mahakama ya Malawi na wenyeji wao kutoka Mahakama ya Tanzania.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Kifungu Kariho akizungumza jambo na washiriki wa kikao kazi cha mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika ya Mahakama ya Juu ya Malawi na Mahakama ya Tanzania.
(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni