Jumatatu, 23 Septemba 2024

MAHAKAMA SPORTS CLUB KAMA ‘NUNGUNUNGU’ MASHINDANO YA SHIMIWI

Na EVELINA ODEMBA – Mahakama Morogoro

 

Timu zinazounda Mahakama Sports Club zageuka kuwa mwiba mkali unaofananishwa na Nungunungu katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea mjini Morogoro.

 

Mwiba huu unaonekana baada ya jana tarehe 22 Septemba, 2024 Mahakama kuendelea kupata ushindi mfululizo kuanzia mashindano hayo yalivyoanza tarehe 18 Septemba, 2024.

 

Timu ya Kamba Wanaume (ME) toka Mahakama imeiburuza Ras Shinyanga kwa kuivuta mara mbili wakati kwa upande wa wanawake, Mahakama imejitwalia ushindi wa kuwavuta UCSAF.

 

Kwa upande wa mpira wa pete, bado Mahakama imetoa miiba yake na kuichoma Ras Lindi kwa magori 41 kwa 10 waliyojifutia damu, hatua hii inapelekea Mahakama kuendelea kuwa tishio katika Mashindano haya.

 

Licha ya Mahakama kuwa na jukumu zito la kutoa haki, lakini bado imeendelea kufanya vizuri katika michezo na hii ni kutokana na kuwa na ushirikiano mzuri baina ya watumishi.  

 

Katika timu zinazounda Mahakama Sports Club kuna watumishi wa kada mbalimbali ambao wanashirikiana kuonesha vipaji vyao ili kuipatia sifa njema ya ushindi Mahakama ya Tanzania.


Timu ya kuvuta Kamba ya wanawake (KE) toka Mahakama Sports Club ikiwa katika harakati za kuwavuta USCAF (hawapo pichani).


Timu ya kuvuta Kamba ya wanawake (KE) toka Mahakama Sports Club ikishangilia ushindi wake dhidi ya USCAF.


Timu ya kuvuta Kamba ya wanaume(ME) toka Mahakama Sports Club ikitetea ushindi wake dhidi ya RAS  Shinyanga.

Timu ya kuvuta Kamba ya wanaume(ME) toka Mahakama Sports Club ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuiburuza RAS Shinyanga.

Timu ya Mpira wa Pete toka Mahakama Sports Club ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wake dhidi ya RAS Lindi.

Timu ya Mpira wa Pete toka Mahakamani ikiwa dimbani.

Mchezaji wa Mahakama, Tatu Mawazo akiifungia Mahakama bao dhidi ya RAS Lindi.

Benchi la Ufundi toka timu ya mpira wa Pete ya Mahakama Sports ikifuatilia kwa makini mchezo uliokuwa ukiendelea uwanjani.

Ubao wa Matangazo ukiendelea kutangaza ushindi wa Mahakama.

Matokeo ya mwisho mara baada ya Mahakama kujinyakulia ubingwa mnono.


Mashabiki wa Mahakama Sports wakishangilia kwa fufaha wakati timu yao ya Mpira wa Pete ikiiwaajibisha RAS Lindi.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni