Na EVELINA ODEMBA – Mahakama, Morogoro
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Morogoro, Mhe. Latifa Mansoor amewahimiza watumishi wa Mahakama katika Kanda
yake kuendelea kuchapa kazi mwaka mpya 2025.
Mhe. Mansoor alitoa wito huo hivi karibuni katika
hafla fupi ya kuupokea mwaka 2025 na kuwapokea watumishi wapya iliyofanyika
katika viwanja vya Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki.
“Tunamshukuru Mungu kwa kutuvusha salama, natamka
rasmi kauli mbiu yetu kwa mwaka 2025 ni kazi kazi kazi. Kila mmoja akaze
mkanda kuhakikisha tunatimiza malengo yetu yote tuliyojiwekea,” alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mtendaji wa Mahakama Morogoro,
Bw. Ahmed Ng’eni aliwahuimiza watumishi kuendelee kuzingatia maadili na
taratibu za kiutumishi ikiwemo kufika kazini kwa wakati na kuwa na huduma nzuri
kwa wateja.
Katika hafla hiyo, watumishi wapya ambao ni ajira mpya
pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe.
Janeth Boazi walitambulishwa.
Mhe. Boazi alitumia wasaa huo kuomba ushirikiano
thabiti ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi huku akihaidi
kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha Kanda ya Morogoro inafanya kazi kwenye
viwango bora.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Latifa Mansoor (kushoto) akisalimiana na Viongozi wa Mahakama wakati akiwasili katika Kituo chake cha kazi mara baada ya likizo yake kutamatika. Kushoto ni Mtendaji wa Mahakama, Bw. Ahmed Ng’eni, akifuatiwa na Naibu Msajili, Mhe. Susan Kihawa na wa tatu kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mhe. Janeth Boazi.
Baadhi ya watumishi wa Mahakama wakifuatilia nasaha za Viongozi katika kuupokea mwaka 2025.
Keki maalumu iliyoandaliwa kama kiashiria cha kuanza mwaka 2025 kwa Mahakama Kanda ya Morogoro.
Naibu Msajili, Mhe. Susan Kihawa akisililiza maoni mbalimbali yaliyoandikwa na watumishi wa Mahakama ikiwa ni sehemu ya kuanza mwaka 2025.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Janeth Boazi akijitambulisha mbele ya Viongozi na watumishi wa Mahakama.
Sehemu ya watumishi wa Mahakama ambao ni ajira mpya wakijitambulisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni