Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma
Uongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhe. Barke Sehel jana tarehe 09 Januari, 2024 walikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Wakiwa katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Viongozi hao walipata fursa ya kumueleza Makamu wa Rais kuhusu historia, malengo pamoja na mikakati ya Chama hicho.
Aidha walieleza kuwa, Dira kuu ya TAWJA ni kukuza haki za binadamu na usawa kwa wote. Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inalenga kuwa na mifumo imara ya kisheria na kitaasisi na kwamba TAWJA inaangazia zaidi kukuza haki na usawa kwa wanawake, watoto na makundi mengine hatarishi kama wazee.
Walimueleza Kiongozi huyo kwamba, TAWJA ina Mpango Mkakati wake wa miaka mitano ulioainisha maeneo 10 muhimu ya ufuatiliaji hadi kufikia mwaka 2028/2029 ambayo maeneo hayo ni pamoja na kukuza Haki za Binadamu na usawa kwa wote hasa kwa wanawake, wasichana na makundi mengine hatarishi nchini Tanzania Bara na Zanzibar, kukuza upatikanaji wa haki kwa wanawake wote.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za Viongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) walipokutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni