Na Daniel Sichula – Mahakama, Mbeya
Jaji
wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Winifrida B. Korosso ameongoza kikao cha
tathmini ya vikao vya vya Mahakama ya Rufani Tanzania Mbeya vilivyoanza mnamo
wa tarehe 10 February, 2025 hadi tarehe 28 February, 2025 ikiwa mashauri 25
kati ya 26 yamesikilizwa na kuamuriwa na shauri 1 limehairishwa na kufika
malengo kwa asilimia 96 ya mashauri yaliyopangwa.
Aidha,
Mhe. Korosso ambaye alikuwa Mwenyekiti wa jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani
waliosikiliza wa mashauri hayo kwa kushirikiana na Majaji wengine wa Mahakama
hiyo ambao ni Mhe. Panterine M. Kente na Mhe. Leila E. Mgonya kwa pamoja walisikiliza
mashauri ya Jinai 16 na Mashauri ya Madai 10 na mashauri 12 yametolewa hukumu
na mashauri 13 yatatolewa uamuzi tarehe 28 February, 2025.
Akieleza
sababu moja wapo ya mafanikio hayo, Mhe. Korosso aliwashukuru Jeshi la Magereza
jijini Mbeya kwa kuwawaisha wafungwa mapema Mahakamani na Mawakili kwa ujumla
kufika mapema kumewarahisishia wao kufanya kazi kwa urahisi na kumaliza
mashauri mapema.
“Niwapongeze
Jeshi la Magereza, Mawakilia wa Serikali na wa kujitegemea, Ofisi ya Waendesha
Mashtaka na Wadawaa wengine kwa kufika kwao mapema Mahakamani kwa wakati wote
wa usikilizaji wa mashauri hayo, naweza kusema mafanikio haya yamechangiwa nanyi
kwa kujitoa kwa wakati wote,” alisema Mhe. Korosso
Wakati
huohuo, Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Kanda ya Mbeya
walieleza changamoto zilizojitokea kwa upande wa Magereza na kwa Mawakili
katika suala la uchelewashaji wa kuleta sababu za nyongeza katika mashauri ya
Rufani pamoja na vitabu vya Rufani kuwa na sababu nyingi za Rufaa zisizokua na
mashiko na kupelekea baadhi ya mashauri kuchelewa kufanyiwa maamuzi, vielelezo
kutosamana na hukumu zinazotolewa hasa kwa Mahakama za Mwanzo.
Kwa
upande wake Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria
Nongwa kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya aliwapongeza
Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa mafanikio waliyopata kwa kipindi chote cha
usikilizaji wa mashauri hayo yaliyokuwa yamepangwa kusikilizwa.
“Tuna
ahidi kwenu kwamba tutaendelea kutembelea Gereza la Ruanda lililopo Mbeya kutoa
elimu ya sheria ili wafungwa waweze kuendelee kuboresha sababu zao za Rufaa
wanazoleta Mahakamani,” alisema Jaji Nongwa.
Naye,
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi.
Mavis Miti pamoja na Mahakimu wa Mahakama Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Mageleza,
Polisi, Mawakili wa Serikali, Mawakili wa kujitegemea, Ofisi ya Mwendesha
Mashtaka wa Serikali kwa nyakati tofauti walilishukuru Jopo hilo la Majaji wa Mahakama
ya Rufani kwa kuendesha mashauri ya Rufani kwa haki, kusaidia kujifunza mambo
mengi katika utekelezaji wa sheria na utoaji haki kwa wananchi kwa wakati.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Winifrida Korosso akifungua Kikao cha tathmini ya uendeshaji wa mashauri ya rufaa ya Mahakama ya Rufani jopo lililoketi Mahakama Kuu Mbeya, kushoto ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Judith Lyimo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Panterine M. Kente (kulia) na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Leila E. Mgonya (kushoto) wakifuatilia kikao cha tathmini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni