Na Daniel Sichula-Mahakama, Mbeya
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya tarehe 24 Februari, 2025 imeungana na Taasisi
zingine za kisheria mkoani Mbeya kwenye uzindua wa Kampeni ya Msaada wa
Kisheria ya Mama Samia katika viwanja vya Stendi ya Daladala Kabwe na kushiriki
kikamilifu katika utoaji wa elimu na msaada wa kisheria.
Katika
banda la Mahakama Mkoa wa Mbeya limejikita katika kutoa elimu ya kisheria kwa
wananchi hususan katika masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi,
mirathi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala.
Aidha, akizungumzia kampeni hiyo Mtaalam
kutoka Wizara ya Katiba na Sheria alifafanua kwamba, lengo la kuanzishwa kwa
Kampeni hiyo ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia ni kulinda na kukuza
upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini na
kampeni hiyo ilianzishwa mwaka 2023 na itaendelea hadi 2026 kwa nchi nzima.
Vilevile, katika kampeni hiyo,
wananchi wa Mbeya wamejitokeza kwa wingi katika mabanda ya Taasisi mbalimbali
ili kupata msaada wa kisheria na imepelekea kampeni hiyo kuongeza uelewa wa
kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususani haki za wanawake na watoto,
ukatili wa kijinsia, masuala ya haki na wajibu na misingi ya utawala bora.
Aidha,
toka Kampeni hiyo imeanza katika mikoa mbalimbali nchini imekua ikigusa moja
kwa moja mambo mbalimbali ya kisheria ya wananchi katika kupata msaada wa
kisheria kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia,
Wanazuoni na Wadau wa Maendeleo.
Watumishi wa Mahakama Wakitoa Elimu ya Sheria kwa Wananchi waliofika Kwenye Banda la Mahakama Kuu Mkoa wa Mbeya
Wananchi wakipata huduma kwenye Banda la Rita
Wananchi wakipata Elimu ya Sheria kwenye Banda la Wizara ya Katiba na Sheria
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni