Na IMAN PATSON MZUMBWE- Mahakama, Songwe
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Songwe pamoja na wadau wa Mahakama Mkoani humo wamefanikiwa
kutembelea shule za Sekondari na Msingi katika kipindi cha maadhimisho ya wiki
ya sheria mwaka 2025, kwa lengo la kutoa elimu juu ya Ukatili wa kijinsia,
Rushwa, Wosia, Mirathi, Muundo wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Nafasi ya
Mahakama ya Tanzania katika kufanikisha dira ya maendeleo ya Taifa 2050.
Hakimu
Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi Mhe. Vitalis Changwe ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Elimu Mkoa aliongoza zoezi hilo la utoaji elimu alisema kuwa,
elimu hiyo itasaidia kupunguza matukio na matendo yasiyokuwa ya kiungwana
katika jamii zetu kwani wanafunzi hao wataweza kusaidia kueneza na kuwaelimisha
wazazi, watoto wengine katika jamii zinazowazunguka.
Aidha,
Maafisa kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe walitoa mada juu ya namna ambavyo
vitendo vya ukatili vinavyoweza kusababisha watoto wengi kutofikia malengo yao
kwenye jamii. Watoto wengi wanafanyiwa vitendo hivyo vya ukatili lakini hawatoi
taarifa popote matokeo yake yanaleta madhara kwa jamii mfano; mimba za utotoni,
magonjwa na kufanyishwa kazi ambazo hawazisitahili bira ridhaa yao.
Aidha,
Vitendo hivyo, vinafanyika kwa sababu wengi wao hawana elimu juu ya ukatili. Ni
wakati sahihi kuwaelimisha wanafunzi nini maana ya ukatili na kuwasisitiza kuwa
wasisite kutoa taarifa pale wanapofanyiwa
au kuona vitendo hivyo vinafanyika kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha
wanafunzi hao kutofikia malengo yao, lakini pia waliwasihi wanafunzi hao kuwa
waende kuwa mabalozi kwa wengeni katika jamii kwani kwa kufanya vitendo vya
ukatili ni kosa kisheria na adhabu ni kifungo jela.
Wakati
huohuo, Maafisa kutoka TAKUKURU Mkoa wa Songwe wametoa elimu kuhusu rushwa na
madhara yake wanafunzi hao kwa nyakati tofauti wakieleza kuwa, vitendo vya
rushwa ni adui namba moja wa haki katika jamii kwasababu inaweza kusababisha
mwenye haki asiipate haki yake anayoitafuta. Rushwa inaweza kusababisha
migogoro baina ya pande mbili na inaweza kufifisha maendeleo katika jamii.
Vilevile,
wamewaelimisha na kuwahimiza wanafunzi hao kuwa waende kuwaelimisha wengine ikiwa pamoja na
wazazi, marafiki na watu wengine juu ya madhara ya rushwa ikiwa ni pamoja na kutotoa
au kutopokea rushwa, kwani kwa kufanya hivyo ni kosa la kijinai na adhabu yake ni kifungo au faini
ama adhabu zote mbili kwa wakati mmjo.
Kamati hiyo ya utoaji elimu imejumuisha wadau kutoka Taasisi mbalimbali kama vile
TAKUKURU, Ofisi ya mashtaka Taifa Mkoa wa Songwe, Jeshi la polisi Mkoa, Ustawi jamii,
Huduma kwa jamii, mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Mbozi na Mawakili wa kujitegemea Mkoa wa Songwe.
Afisa
wa TAKUKURU akiwaelimisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Ephata juu ya madhara yatokanayo na Rushwa katika jamii.
Mmoja
ya mwanafunzi wa shule ya msingi Ephata akitoa neno la shukurani kwa niaba ya
wanafunzi wengine.
Afisa wa Jeshi la Police Bi. Merina Method akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule Msingi Sasenga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni