Na DOTTO NKAJA- Mahakama, Geita
Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Griffin Mwakapeje amefanya ukaguzi wa robo ya tatu ya mwaka 2025 leo tarehe 24 machi, 2025 katika Mahakama ya Wilaya Nyang’hwale na Mahakama za Mwanzo wilayani hapo, ambapo aliwapongeza watumishi wa Mahakama kwa utendaji kazi mzuri.
Lengo la kujua mambo mbalimbali na taarifa za mashauri yaliyofunguliwa, mashauri yaliyoyamalizika, mashauri ambayo bado hawajamaliza kuyasuluhisha,zikiwemo changamoto wanazokumbananazo katika utendaji kazi wa shughuli za kimahakama.
Jaji huyo alifanya ziara hiyo, akiwa ameongozana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Fredrick Lukuna na Mtendaji wa Mahakama hiyo, Bi. Masalu Cosmas Kisasila.
Aidha Jaji Mwakapeje alianza kutembelea Mahakama ya Mwanzo Mwingiro,ambapol aliwapongeza watumishi wa Mahakama hiyo kwa kazi nzuri walioionesha toka mwaka 2024 kwa kumaliza mashauri kwa wakati na kuendana na kasi ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na M awasiliano(TEHAMA) katika uendeshaji wa mashauri.
Vilevile Jaji Mwakapeje alishuhudia changamoto za miundombinu katika Mahakama hiyo na kuwashauri watumishi hao,kuwa wajitahidi kutunza nyaraka za Serikali kwa mazingira salama, ikiwemo kuazingatia suala la maadili maana ndio uti wa mgongo wa Mahakama ya Tanzania.
Amewasistizia kuwa wawe na utaratibu wa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kupunguza changamoto za watu kutofuatilia kesi zao na kuchelewa kuisha.
Baada ya kumaliza ukaguzi katika Mahakama ya Mwanzo Mwingiro, walienda Mahakama ya Mwanzo Kharumwa wilayani Nyang’hale.
Alikagua Mahakama hiyo akiwa na ujumbe huo,ambapo pia wasistiza kuwa uendeshaji wa mashauri ufanyike hatua kwa hatua na kuwaasa wahe.Mahakimu kwamba wahakikishe hukumu zifanyika kwa wakati.
Ujumbe huo ulimaliza ukaguzi huo, kwenye Mahakama ya Wilaya Nyang’hwale na kukagua mashauri yote na kuwapongeza watumishi wote wa Mahakama hiyo kwa kufanya vizuriu katika kumaliza mashauri kwa wakati na kuonekana kuwa wameingia kumi bora nchini katika umalizaji wa mashauri.
Kwa upande wake Mhe. Lukuna aliwapongeza watumishi wa Mahakama ya Nyang’hwale kwa kufanya kazi kwa ushirikiano huku akisema wafuata taratibu na sheria za Mahakama katika kutoa haki kwa wananchi.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda Geita, Mhe.Griffin Mwakapeje akisaini kitabu cha wageni Mahakama ya Mwanzo Mwingiro.
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Geita akitoa maelekezo kwa watumishi kuhusu utekelezaji wa majukumu yao kwa njia ya Tehama.
(Habari hii imehaririwa na MAGRETH KINABO- Mahakama, Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni