Ijumaa, 28 Machi 2025

MENEJIMENTI YA MAHAKAMA MBEYA YAKUTANA

Na Mwinga Mpoli – Mahakama, Mbeya 

Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania Mkoa wa Mbeya jana tarehe 27 Machi, 2025 imefanya kikao cha robo ya tatu mwaka 2024/2025 ili kutathmini utendaji kazi wa mkoa huo.

Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mahakama Kuu Mbeya na Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga. 

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Tiganga aliwataka wajumbe wa kikao hicho kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, pia kuwatia moyo watumishi wa chini na wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

“Ni vyema tukafanya kazi kwa bidii na tuwasimamie watumishi tunaowaongoza wasipotoke kimaadili na tuwatie moyo watumishi wanaofanya kazi katika mazingira magumu haswa wale wa vituo vilivyo vijijini tusiwakatishe tamaa,” alisema Jaji Tiganga.

Vilevile, Mhe. Tiganga aliwaasa wajumbe hao kufanya kazi kwa ubunifu na kukabiliana na changamoto zote zitakazojitokeza na kuhakikisha wanakuwa salama kiafya na kisaikolojia.

Wajumbe wa kikao hicho walipokea taarifa za Mirathi kwa ngazi zote za Mahakama na taarifa za utekelezaji wa shughuli za kimahakama na kiutawala ambapo maazimio mbalimbali yaliwekwa ili kuhakikisha huduma za haki kwa wananchi zinawafikia kwa wakati.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga (katikati) kulia kwake ni Naibu Msajili Mfawidhi Mhe. Aziza Emily Temu na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Bi. Mavis Francis Miti wakiongoza kikao cha menejimenti.

Sehemu ya Wajumbe wa kikao hicho wakisikiliza kwa Makini taarifa zinazotolewa.

Mmoja ya Wajumbe wa kikao hicho akifafanua jambo mara baada ya kusomwa kwa ajenda na taarifa za kikao hicho zinazotolewa. 

Kikao cha robo ya tatu mwaka 2024/2025 kikiendelea

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni