Na ARAPHA RUSHEKE –Mahakama, Dodoma
Mahakama, katika
kutekeleza jukumu lake la kikatiba la utoaji haki kwa mwaka 2024, imefanikiwa
kupunguza mlundikano wa mashauri hadi kufikia asilimia 4 katika miaka minne
mfululizo .
Mafanikio hayo
yamebainishwa leo tarehe 10 April,2025 na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,
Mhe. Eva Nkya alipokuwa anawasilisha taarifa yake kwenye Kikao cha Baraza la
Wafanyakzi Kitaifa linalofanyika katika ukumbi wa PSSF Jijini Dodoma.
Msajili Mkuu amebainisha
pia kuwa, mlundikano wa mashauri umeshuka toka asilimia 11 kwa mwaka 2021 hadi
asilimia 4 kwa mwaka 2024.
Wastani wa jumla wa mzigo
wa kazi ulipungua kutoka mashauri 234 hadi 227. Aliongezea kuwa wastani huo pia
ulipungua katika ngazi zote za Mahakama isipokuwa Mahakama Kuu na Mahakama ya
Rufani.
Ameeleza kuwa katika
kufanikisha mafanikio hayo, Mahakama
ilifanya vikao maalumu vya kuondoa na kuzuia mlundikano wa mashauri katika
ngazi zote za Mahakama isipokuwa Mahakama za Mwanzo.
“Ufunguaji wa mashauri
Mahakama Kuuuliongezeka kwa silimia 11 na kupungua kwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi kwa silimia 24, Mahakama za Wilaya kwa asilimia 6, Mahakama za Watoto
kwa asilimia 9 na Mahakama za Mwanzo kwa asilimia 36,’’alisema Msajili Mkuu.
Aliongezea kuwa umalizaji
wa mashauri uliongezeka kwa Mahakama Kuu kwa asilimia 14 na Mahakama za Watoto
kwa sailimia 3 na kupungua kwa Mahakama za Hakimu mkazi kwa silimia 21,
Mahakama za Wilaya kwa asilimia 3 na Mahakama za Mwanzo kwa asilimia 2.
Mhe. Nkya ameeleza kuwa
utendaji mzuri wa Watumishi wa Mahakama, wakiwemo Majaji na Mahakimu
umesababisha kupungua kwa kiasi kikubwa malalamiko ya Wananchi na kuongeza
Imani katika utoaji haki.
Alimaliza kwa kusema kuwa
wataendelea kuongeza ufanisi wa mifumo ili kuongeza kasi ya usikilizaji wa
mashauri, kuendelea kuchambua kanuni zinazohitaji marekebisho, kusimamia
utekelezaji wa vigezo vya upimaji utendaji na kufuatilia maendeleo ya Dira ya Maendeleo
ya Taifa 2050 ambayo italeta taswira ya Mpango Mkakati wa Mahakama unaokuja.
Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni