Na Christopher Msagati- Mahakama, Manyara
Wanafunzi
wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro
wamefanya ziara ya kujifunza shughuli na taratibu mbalimbali za kimahakama,
Mahakama Kuu Manyara.
Ziara
hiyo, iliyofanyika leo tarehe 21 Mei, 2025 jumla ya wanafunzi Hamsini na tatu (53)
kutoka Chuo hicho waliambatana na walimu wao watatu (3) kwa lengo la kujifunza
taratibu na masuala mbalimbali yanayotendeka mahakamani kwa njia ya vitendo ili
kuwasaidia katika elimu wanayojifunza chuoni.
Akizungumza
katika mafunzo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mhe.
Karimu Mushi, amewafundisha wanafunzi hao juu ya taratibu mbalimbali za usikilizwaji
wa mashauri yanayohusu Wanyamapori kuanzia hatua ya kwanza yanapofunguliwa,
kusikilizwa na hata hatua ya mwisho ya utoaji wa Hukumu.
Aidha,
Mhe. Mushi aliwasisitiza wanafunzi hao, kujitahidi kuhudhuria mahakamani mara
kwa mara kwa sababu kujifunza kwa vitendo kuna tija zaidi kuliko kujifunza kwa
nadharia pekee.
“Chuoni
mnasoma zaidi kwa nadharia, nawapongeza kwa kuja leo na kushuhudia namna ya
mashauri haya yanayohusu wanyamapori yanavyoendeshwa mahakamani. Mafunzo haya
yataongeza tija na uelewa wenu zaidi katika hayo mnayojifunza chuoni,” alisema
Mhe. Mushi.
Naye,
Hakimu Mkazi na Msaidizi wa Sheria wa Jaji wa Mahakama Kuu, Manyara Mhe.
Thobias John alitumia nafasi hiyo kuwafundisha wanafunzi hao juu ya Muundo wa
Mahakama ya Tanzania ulivyo.
“Mahakama
zetu hapa nchini, kuanzia Mahakama ya Mwanzo, Mahakama za Wilaya na Mahakama za
Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu Pamoja na Mahakama ya Rufaani zina taratibu zake za
usikilizaji wa mashauri kulingana na uzito wa mashauri husika hivyo ni vema
mkafahamu kuwa hata haya mashauri ya Wanyamapori mathalani hayawezi kusikilizwa
katika ngazi za Mahakama za Mwanzo,” amesema Mhe. Thobias John.
Mwendesha
Mashtaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Bw. Rusticus Mahundi,
aliwapongeza wanafunzi hao kwa kuchagua Mahakama Kuu Manyara kwa ajili ya
kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu taratibu za kimahakama.
“Mmefanya
jambo sahihi kuichagua Mahakama hii kwa sababu mashauri mengi yanayohusu
wanyamapori yanashughulikiwa hapa kutokana na sababu za uwepo wa Mbuga za
Wanyama na Mapori mengi ya akiba ambapo makosa mengi yanayohusu wanyamapori
yanafanyika,” alisema Bw. Mahundi.
Kwa
upande wake, mwakilishi wa Walimu waliombatana na wanafunzi hao Dkt. Emanuel
Martin baada ya mafunzo hayo aliushukuru uongozi wa Mahakama Kuu Manyara kwa
kuwapokea vema na kuwapa Elimu waliyokuwa wakiihitaji.
“Tunashukuru
sana Uongozi wa Mahakama Kuu Manyara kwa kutupokea na kwa ushirikiano mliotupa,
tuaamini kuwa elimu hii itatusaidia sana na tutaendelea kuja hapa kwa ajili ya
mafunzo mengine” alisema Dkt. Martin.
Mahakama
Kuu, Kanda ya Manyara imeendelea na utaratibu wa kutoa elimu kwa kwa wananchi wanaofika mahakamani
kila wakati lakini pia kwa kupitia vyombo vya Habari vilivyopo hapa mkoani kwa
lengo la kuendeleza mahusiano bora kati ya Mahakama na wadau wanaosaidia utekelezaji
wa shughuli mbalimbali za Mahakama.
Wanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka wakiwa wakiwa nasikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali katika ziara yao ya Mafunzo Mahakama Kuu Manyara iliyofanyika leo tarehe 21 Mei, 2025.
Wanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka wakiwa wakiwa nasikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali katika ziara yao ya Mafunzo Mahakama Kuu Manyara iliyofanyika leo tarehe 21 Mei, 2025.
Wanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka wakiwa wakiwa nasikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali katika ziara yao ya Mafunzo Mahakama Kuu Manyara iliyofanyika leo tarehe 21 Mei, 2025.
Hakimu Mkazi wa Mahakama Kuu Manyara ambaye pia ni Katibu wa Sheria wa Jaji Mhe Thobias.K.John akitoa Mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka ( hawapo pichani) waliofika Mahakama Kuu Manyara kwa ajili ya ziara ya Mafunzo.
Hakimu
Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mhe. Karimu Mushi akitoa Mafunzo kwa
wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (hawapo pichani) waliofika Mahakama Kuu Kanda ya Manyara kwa ajili ya ziara ya Mafunzo leo tarehe 21 Mei, 2025.
Mwendesha Mashtaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Bw. Rusticus Mahundi akizungumza na wanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka (hawapo pichani) waliofika Mahakama Kuu Manyara kwa ajili ya ziara ya Mafunzo.
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni