- ·Apongeza kasi ya uondashaji wa Mashauri
Mahakamani
- ·Awaasa watendaji kukaza buti kwenye matumizi ya TEHAMA
- ·Asisitiza kufanya kazi kwa uadilifu
Na. Hilary Lorry – Mahakama, Lindi
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara,
Mhe. Saidi Dingo’hi amefanya ziara ya ukaguzi katika Mkoa wa Lindi na kukagua
Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mahakama za Wilaya tano (5) za Mkoa wa Lindi, Mahakama
ya Wilaya ya Lindi, Kilwa, Liwale, Ruangwa, Nachingwea na Mahakama za mwanzo
zilizopo katika Mkoa huo.
Akizungumza
na watumishi wa Mahakama kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo Mhe. Dingo’hi
alisema nimeshuhudia kazi nzuri mnayofanya alipokuwa akikagua Mahakama za
Wilaya hizo na kuwakumbusha watumishi kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu wa
hali ya juu.
Aidha,
Mhe. Dingo’hi aliwapongeza watumishi katika mkoa huo kwa kuchukua jitihada za
makusudi katika ufanyaji wa kazi kwa bidii hasa Mahakimu kwa kusikiliza mashauri kwa wakati bila kuzalisha mashauri ya muda mrefu (mashauri
ya Mlundikano) na kutokuwa na mashauri
mengi yanayoendelea mahakamani (pending cases) hiyo ni kutokana na kasi ya
usikilizaji na umalizaji wa mashauri kwa wakati.
“Nawapongeza
Mahakimu wote kwa kutekeleza jukumu lenu
la msingi la usikilizaji na uondoshaji
wa Mashauri kwa wakati lakini pia niwatake mtekeleze jukumu hilo kwa uadilifu
ili haki isionekene tu bali ionekane ikitendeka hii itarejesha imani ya jamii
kwa Mahakama” alisisitiza Jaji Dingo’hi.
Aidha,
Mhe. Dingo’hi aliwaasa watumishi katika mkoa huu kuachana kabisa na matumizi ya
karatasi na kujikita zaidi katika
matumizi ya Mifumo ya TEHAMA, pamoja na mifumo
ya uratibu wa Mashauri na Mifumo Mingene yote iliyoanzishwa au kutumiwa na Mahakama
ya Tanzania kwani lengo ni kurahisishia utekelezaji wa majukumu ya kila
siku.
Vilevile,
Mhe. Dingo’hi aliwataka watumishi kuwachukulia wateja wote kwa usawa bila kujali vyeo vyao, hadhi zao hili kuwachukulia kwa usawa Mawakili wa
Serikali na Mawakili wakujitegemea vyivyo hivyo.
Aidha,
Jaji Dingo’hi aliwataka watumishi kuendelea kuleana kielimu (Mentorship) ikiwa
ni mwendelezo wa utekelezaji wa agizo la Jaji Mfawidhi Kanda ya Mtwara
Mhe.Edwin Kakolaki.
Mhe.Dingo’hi
pia alitembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi (IJC) Lindi pamoja
na gereza la Wilaya ya Lindi.
Kwa
upande wao viongozi wengine walioambatana na Jaji Dingo’hi katika ziara hiyo ya
ukaguzi ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara Mhe. Seraphina
Nsana, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Lindi Mhe. Consolata Peter Singano,
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara Bw. Yusuph Msawanga na
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Mbeyela kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo
waliwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa nidhamu.
Jaji
wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara Mhe.Saidi Dingo’hi (katikati)
akiteta Jambo na watumishi (hawapo kwenye picha) wakati wa ziara ya ukaguzi.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe.Consolata Peter Singano akisoma
taarifa ya Mahakama ya Mkoa wa Lindi Mbele ya Mhe.Jaji Dingo’hi.
Mtendaji wa Mahakama Kuu kanda ya Mtwara Bw. Yusuph Msawanga akiteteta jambo na watumishi katika ziara hiyo ya ukaguzi.
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Godfrey Mbeyela akieleza jambo wakati wa ukaguzi.
Jaji
wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara Mhe. Saidi Dingo’hi akipanda Mti wa
Kumbukizi alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Mandawa iliyopo Wilaya ya Ruangwa.
Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi wakiwa katika Picha ya pamoja na Jaji wa mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Saidi Dingo’hi (aliyesimama katikati).
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara Mhe Saidi Dingo’hi na Jopo lake wakionyeshwa mwenendo wa Ujenzi wa Mradi wa chumba cha Mahakama Mtandao kinajojengwa Gereza kuu Lindi.
Picha ikionyesha zoezi la ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa kituo Jumuishi
(IJC) Lindi.
Watumishi
wa Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa wakiwa katika Picha ya pamoja na Jaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Saidi Dingo’hi wakati wa ziara yake ya
ukaguzu wilaya ya Ruangwa.
Picha ikionyesha zoezi la ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa kituo Jumuishi
(IJC) Lindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni